Marekani yaandaa vikwazo vipya dhidi ya Iran

  • Habari NO : 809261
  • Rejea : abna.ir
Brief

viongozi wa Iran wamejibu Trump wakisema kuwa: viongozi wote waliomtagulia walikuwa wanashindana kuipa vikwazo Iran na kufanya uadui dhidi ya Iran lakini wote wameondoka bila ya kuiathiri Iran na badala yake vikwazo vimekuwa sababu ya Iran kupata maendeleo na kujitegemea zaidi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Maafisa nchini Marekani wamesema utawala wa Trump unajiandaa kuiwekea vikwazo vipya Iran, katika hatua ya kwanza ya kuiadhibu nchi hiyo tangu ikulu ya White House ilipoionya Iran kufuatia jaribio lake la kombora la masafa marefu. Zaidi ya watu na makampuni 20 na yumkini mashirika ya serikali huenda yakajumlishwa katika hatua hiyo, wamesema maafisa na watu wengine walio na ufahamu kuhusu uamuzi huo. Vikwazo hivyo vinavyokuja katika wiki za kwanza za utawala wa Trump, vinaakisi shauku ya utawala huo kuchukuwa msimamo mkali dhidi ya Iran kuanzia mwanzo. Wakati wote wa kampeni zake, Trump aliutuhumu utawala wa mtangulizi wake Barack Obama, kwa kutokuwa na msimamo mkali dhidi ya Iran, na kuahidi hatua kali atakapochaguliwa. Ikulu ya White House na wizara ya mamo ya nje zilikataa kuzungumzia suala hilo, jana. Lakini Trump aliishambulia Iran kupitia ukurasa wake wa twita akisema "wanacheza na moto," na kwamba hatokuwa na huruma nao kama alivyofanya Obama.

Wakati huo viongozi wa Iran wamejibu Trump wakisema kuwa: viongozi wote waliomtagulia walikuwa wanashindana kuipa vikwazo Iran na kufanya uadui dhidi ya Iran lakini wote wameondoka bila ya kuiathiri Iran na badala yake vikwazo vimekuwa sababu ya Iran kupata maendeleo na kujitegemea zaidi.

Iran imesisitiza kuwa haitegemei Marekani na wala haikuwa ikitegemea Marekani, na imeahidi kujibu kila aina ya uadui utaofanywa na serikali ya Trump.

Mwisho wa habari/ 291


Taarifa zinazohusiana

Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

پیام رهبر انقلاب به مسلمانان جهان به مناسبت حج 1441 / 2020
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni