Ujumbe muhimu wa kiongozi mwadhamu wa mapinduzi ya Iran kwa Waislamu ulimwenguni na mahujaji mwaka 2016

  • Habari NO : 777052
  • Rejea : ParsToday
Brief

Kiongozi mwadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: ulimwengu wa Kiislamu pamoja na nchi zake wanapaswa kuwafahamu vyema viongozi wa Saudi Arabia, kufuatia jinai walizoeneza katika mataifa ya Kiislamu, hivyo hatupaswi kuwaachia usimamizi wa Ibada ya Hija wao pekee na tunapaswa tutafakari kuhusu njia mbadala ya kuisimamia Haram mbili na ibada ya Hija.

Shirika la habari Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hivi sasa tukiwa karibu na masiku ya msimu wa Hija, Ayatullah Kamanei kiongozi wa mapindi ya Kiislamu ya Iran, ametoa ujumbe muhimu kwa Waislamu wote duniani na waliokwenda kuhiji katika nyumba ya mwenyezi Mungu katika mji mtukufu wa Maka, naye ameashiria kuwa Hija ya Ibrahim ni jambo linalodhihirisha utukufu na adhama ya uma wa Kiislamu katika kukabiliana na ubeberu wa kimataifa, katika ujumbe huo ameashiria tukio zito la majonzi na simanzi la Mina, na kuwaeleza Waislamu wote kuwa: ulimwengu wa Kiislamu pamoja na nchi zake wanapaswa kuwafahamu vyema viongozi wa Saudi Arabia, kupitia jinai walizoeneza katika mataifa ya Kiislamu, hivyo basi hatupaswi kuwaachia usimamizi wa Ibada ya Hija wao pekee na tunapaswa tutafakari kutafuta njia mbadala ya kuisimamia Haram mbili na ibada ya Hija kwa ujumla.
Na hapa twanukuu asili ya ujumbe
Kwa jina la mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu, na himidi zote ni za mwenyezi Mungu mlezi wa walimwengu na rehema na amani ziwe kwa mtukufu Muhammad (s.a.w.w) na Ali zake watwaharifu na masahaba wote walio wema na kila aliowafuata kwa wema mpaka siku ya malipo.
Ndugu Waislamu kote duniani!
Msimu wa Hija kwa Waislamu, ni msimu wa fahari na utukufu kwa viumbe, pia ni msimu wa nyoyo kupata Nuru na unyenyekevu kwa Mola muumba. Hija ni ibada takatifu ya kiroho na yakidundia na ya kibinadamu. Ambayo imepatikana kupitia amri ya Allah aliposema «فَاذکُرُوا اللّهَ کَذِکرِکُم ءابآءَکُم اَو اَشَدَّ ذِکرًا» basi mkumbukeni mwenyezi Mungu kama mnavyo wakumbuka baba zenu au zaidi yake (2:200) aidha aliposema «وَ اذکُرُوا اللّهَ فی اَیّامٍ مَعدوداتٍ» na mumdhukuru Allah ndani ya masiku machache (2:203) na katika umpande mwingine akielezea nyanja zisiokuwa na kikomo katika ibada hiyo akasema « ِ الَّذي جَعَلْناهُ لِلنَّاسِ سَواءً الْعاكِفُ فيهِ وَ الْبادِ » (msikiti) ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa kwa waliopo humo au kwa walio nje (22:25).
Katika ibada hiyo isio na kifani jambo la msingi la awali ni kuwa na amani katika kila sehemu na wakati wote, amani ambayo itakuwa kama nyota inayo ngara ambapo amani hiyo hupelekea kupata utulivu nyoyo za wanadamu na mahujaji, kutokana na kuzingirwa na hali ya kutokuwa na amani inayo sababishwa na madhalimu, kama hali hiyo inavyotishia maisha ya mwanadamu pia kuwepo kwa amani na utulivu humfanya mwanadamu huyo kuonja ladha ya amani katika kipindi hicho.
Hija ya Nabii Ibrahim ambayo Uislamu umewazawadia Waislamu ni sehemu ya kudhihiri utukufu na uchamungu na umoja baina ya Waislamu, adhama ya Uma wa Kiislamu na kutegemea kwao nguvu ya milele ya kiungu ambako kunadhihirisha nafasi ya Waislamu, na kuwaweka mbali na wanaosababisha ufisadi katika jamii, udhalilishaji na udhoofishaji ambao mabeberu wa kimataifa huzibebesha jamii za kibinadamu. Hija ya Kiislamu ya kumpwekesha mwenyezi Mungu pia ni sehemu ya kudhihiri neno la Mungu «اَشِدّآءُ عَلَی الکُفّارِ رُحَمآءُ بَینَهُم» kwa maana ni tishio kwa makafiri huku wakihurumiana baina yao (29:25).   Vilevile Hija ni sehemu ya kuwalaani na kujitenga na washirikina na kuleta upendo na umoja baina ya waumini  
Wale wote wanaoamini kuwa Hija ni safari za furaha, mapumziko na pikiniki, huku wakilichukia taifa na waumini wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kuifanya ibada ya hija kuwa ni suala la kisiasa kwa maficho, ni vifaranga vya shetani ambavyo vinajiathiri kwaajili ya kuogopa kuhatarisha mapato mafanikio ya shetani wao mkubwa Marekani. Mwaka huu watawala wa Saudi Arabia imezuia watu kuiendea njia ya mwenyezi Mungu na msikiti mtukufu wa Makka, kwa maana waumini wa Taifa la Iran wamezuiliwa kwenda katika nyumba ya muumba wao, wapotoshaji wanayafanya hayo kwaajili ya kubaki katika viti virefu na nguvu ya kidhalimu ili kulinda maslahi ya mabeberu wa kimataifa na kushikamana na Wazayuni na Marekani na kutekeleza yale yote yanayoamuriwa na tawala hizo.     
Mpaka sasa yakaribia mwaka baada ya kutokea tukio la kusikitisha la Mina ambapo katika tukio hilo maelfu ya waumini wamepoteza maisha siku ya Idi wakiwa ndani ya Ihramu katika jua kali wakiwa na kiu kisio na mfano walipoteza maisha yao katika hali hiyo, pia kabla ya tukio hilo kwa siku kadhaa katika msikiti wa Makka walipoteza maisha yao wakiwa katika hali ya kumuabudu mola wao, viongozi wa Saudi Arabia wanahusika na matukio yote hayo, kwani watu wote walioshuhudia tukio wanathibitisha suala hilo, hata wengine wamefika kusema kuwa matukio hayo yalipangwa makusudi. Uzembe ulifanyika katika kuokoa waliokuwa wanakaribia kukata roho, wakiwa wanatapatapa na kufariki katika sikukuu ya kuchinja huku wakimdhukuru Mungu, hayo yote yanathibitishwa na waliokuwa wanashuhudia tukio hilo. Watawala wa Saudi Arabia waliokuwa na roho ngumu madhalimu baada ya kuwatoa katika sehemu ya tukio waliwaweka katika makontena hatimaye kufunga milango yake, kwa maana  badala ya kuwatibu waliokuwa wamezimia na kuwasaidia walau kwa kuwapa maji, walikufa kishujaa katika hali hiyo. Maelfu ya familia za wahanga wa tukio hili la kusikitisha kutoka mataifa mbalimbali wamepoteza wapendwa wao huku mataifa hayo yakiwa katika maombolezo. Nchi ya Iran pekee imepoteza watu takriban miaka tano, familia zao mpaka sasa wako katika majonzi na maombolezo wakishirikiana na mataifa yao.         
Viongozi wa Saudi Arabia wamefikia hatua hii kwamba baada ya kuomba msamaha na kujuta na kuwahukumu waliohusika mojakwamoja na tukio, kwa masikitiko makubwa bila ya aibu wamekataa na kupinga hata kuunda tume ya kimataifa ya kuchunguza uhakika wa tukio hilo liliounguza nyonyo za waumini, hivyo basi baada ya wao kuwa katika upande wa mtuhumiwa, wakajifanya kuwa ndio wanaotuhumu na  kudhihirisha uadui wao wa kale na serikali ya Kiislamu ya Iran, nakupinga kila bendera iliosimama katika kukabiliana na ubeberu na ukafiri wa kimataifa, utawala huo ulionekana kuungana na makafiri hao katika kuwapinga Waislamu.
Propaganda zao huzieneza kwa kutumia wanasiasa ambao wenye mwenendo unaotia aibu na fedheha katika ulimwengu wa Kiislamu, na mamufti wasiokuwa na usafi wa kiroho wanaokula haramu ambao kwa wazi hutoa fatuwa zinazopingana na Qur`an na sunna za bwana Mtume, ili watumishi wao kwa vyombo vya habari kusambaza mambo hayo bila ya kusutwa na uwepo wao kuhusu uzushi huo. Kwa hakika wanafanya juhudi zisiozaa matunda kwa kuituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuizuia kutoshiriki ibada ya hija mwaka huu. Viongozi hao wafitinishi wametengeza vikundi vya kuwakafirisha Waislamu wengine na kuvipa silaha vikundi hivyo, vimeuingiza ulimwengu wa Kiislamu katika vita vya ndani na kuuwa na kujeruhi watu wasiokuwa na hatia, ambapo wanamwaga damu nchini Yemen, Iraq, Syria na Libya na baadhi ya mataifa mingine, wanasiasa wasiomjua Mungu na kumwogopa wanafanya urafiki na utawala wa kiuvamizi wa Israel na kufumbia macho mateso wanayopata Wapalestina, huku wakiendelea kueneza dhulma na ukandamizaji mpaka katika vijiji na wilaya za Bahrain, viongozi wasio na dini waliofanya tukio kubwa la Mina kwa jina la watumishi wa Haramain, wamevunja utukufu wa Haram ya amani ya mwenyezi Mungu ambapo wageni wa Allah wauliwa katika siku ya sikukuu Mina na kabla ya hapo katika msikiti mtukufu wa Makka, mpaka sasa bado wanadai kuwa ibada ya Hija haijafanywa kuwa ni jambo la kisiasa, huku wakiwatuhumu wengine kwa kutenda dhambi kubwa ambazo wao ndio wamezifanya au ndio wasababishaji. Wao ndio mfano wa wazi wa maelezo ya Qur`an tukufu ambayo imesema “وَ اِذا تَوَلّیٰ سَعیٰ فِی الاَرضِ لِیُفسِدَ فیها وَ یُهلِکَ الحَرثَ وَ النَّسلَ وَ اللّهُ لا یُحِبُّ الفَساد * وَ اِذا قیلَ لَهُ اتَّقِ اللّهَ اَخَذَتهُ العِزَّةُ بِالاِثمِ فَحَسبُهو جَهَنَّمُ وَ لَبِئسَ المِهاد “Na anapo tawala, hufanya juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. Na mwenyezi Mungu hapendi ufisadi. Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi.  Basi huyo inamtosha Jahannam ambapo ni mahala paovu zaidi kwa mapumziko (2:205-206).
Mahujaji wa Iran na wengine kutoka mataifa mengine wamezuiliwa kufanya ibada ya Hija, ambapo ripoti ya mahujaji wa mwaka huu zinaonyesha kuwa ukiachana na kufunga sehemu zisiokuwa kawaida yake kufungwa, wamefunga vyombo vya kijasusi wakisaidiana na serikali ya Marekani na Israel na kuifanya nyumba ya mwenyezi iliokuwa na amani, kutokuwa na amani. Ulimwengu wa Kiislamu na serikali za Kiislamu zinapaswa kuwafahamu kiundani viongozi wa Saudi Arabia na undani wao wa kutokuwa na imani na kupenda dunia, Waislamu wote wanapaswa kufahamu uhalisia wa utawala huo kutokana na kusambaza jinai katika ulimwengu wasijishirikishe naye, pia kutokana na miamala mibaya wanayowafanyia mahujaji, nchi za Kiislamu zinapaswa kutafakari katika kusimamia na kuongoza mahujaji katika haramu mbili tukufu pia kuongoza suala zima la Hija. Na kama watazembea katika kufanya hilo, bila shaka mustakabali wa uma wa Kiislamu utakuwa mbaya zaidi ya haya yaliotufika.     
Ndugu Waislamu mwaka huu kuna pengo kubwa la mahujaji wa Iran katika ibada ya Hija, lakini wao wamehudhuria katika ibada hiyo kwa nyoyo na roho zao, wakishirikiana na mahujaji wengine kutoka pembe zote duniani huku wakihofia hali ya amani ya mahujaji, hivyo wako katika hali ya kuomba dua kwamba familia iliolaaniwa na matwaghuti wasiwadhuru mahujaji hao, kwaajili hiyo ndugu mahujaji nanyi mwapaswa kuwakumbuka na kuwaombea ndugu zenu wa Iran pia kwaajili ya kutokwa na majanga katika jamii ya Kiislamu na kushindwa tawala za kibeberu na kizayuni katika kuwadhuru waumini wa Kiislamu katika nchi za kiisalimu dua zenu zinahitajika.
Nami natoa rambirambi kwa mashahidi waliofariki Mina na Masjidil Haram mwaka uliopita na mashahidi wa Makka (1) na namuomba mwenyezi Mungu mtakatifu awasamehe madhambi yao na kuwatakia utukufu na daraja ya juu mbele ya mola muumba na salamu zetu na amani ziwe kwa Swahibu wa zama hizi kwani dua yake mtakatifu huyo ndio yenye kukubalika kwaajili ya uma wa Kiislamu na kuwaokoa Waislamu katika fitina na shari za maadui wake.

Kwa mwenyezi Mungu ndiko kwenye Tawfiq  
Sayyed Ali Khamanei
2/9/2016

(1)Jinai za Ijumaa ya mauaji ya Makka, ni moja ya mfano mwingine unaoashiria ugomvi wa serikali ya Marekani ambapo tukio hilo lilitokea mwezi 6 mfungo tatu mwaka 1407 katika ibada ya Hija baada ya waumini  kuonyesha kujitenga na washirikina, ambapo viongozi wa Saudi Arabia walifanya jinai hizo na kuivunjia heshima Haram ya mwenyezi Mungu ya amani, ambapo zaidi ya mahujaji 400 waliuwawa kwa kupigwa risasi na wengine wengi kujeruhiwa ambapo asilimia kubwa ya waliouwawa ni wanawake.

mwisho wa Hbari/290


Tuma maoni

Email yako haiwezi kutuma, tafadhali chunguza Email yako

*

Sehemu maalumu ya mashujaa Makamanda wa Kislamu Haji Qassim Soleimani Na Abumahdi Almuhandisi
We are All Zakzaky
Hatuukubali muamala wa Karni