Main Title

source : parstoday/ABNA24
Jumapili

31 Januari 2021

13:17:10
1110951

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu azuru haram tukufu ya Imam Khomemeini (M.A)

Sambamba na kuanza maadhimisho ya alfajiri kumi na katika kukaribia maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi mtukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo asubuhi amezuru katika haram tukufu la mwasisi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuenzi kumbukumbu ya imamu huyo adhimu wa taifa la Iran kwa kusali na kusoma Qurani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amezuru makaburi ya mashahidi wakuu watajika yaani Beheshti, Rajaei, Bahonar na mashahidi wa tukio la tarehe 7 mwezi Tir mwaka 1360 Hijria shamsiya na kumuomba Mwenyezi Mungu awainue waja wake hao. Ayatullah Khamenei amezuru pia makaburi ya mashahidi mashuhuri na kuziombea roho takatifu za watetezi hao wa Uislamu na Iran. 

Leo Jumapili tarehe 12 Bahman sawa na tarehe 31 Januari mwaka 2021 Miladia ni siku ya kuanza Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 

Miaka 42 iliyopita katika siku kama ya leo, yaani tarehe 12 mwezi Bahman mwaka 1357 Hijria Shamsiya sawa na Februari Mosi mwaka 1979 Miladia Imam Khomeini (M.A) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kuwa uhamishoni na mbali na nyumbani kwa miaka 14 alirejea katika Iran ya Kiislamu na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi. 

342/