Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Februari 2021

12:20:01
1113060

Maelfu waandamana kwa siku ya pili Myanmar kulalamikia mapinduzi ya kijeshi

Makumi ya maelfu ya wananchi wa Myanmar wameandamana kwa siku ya pili mtawalia katika mji wa Yangon moja ya miji muhimu ya nchi hiyo licha vitisho vya jeshi na hatua ya utawala wa kijeshi nchini humo ya kukata mawasiliano ya intaneti.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Waandamanaji hao wamesikika wakipiga nara “tunapinga udikteta wa kijeshi’ huku wakiwa wakiwa wamebeba picha za Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala nchini humo cha NLD na kuvaa nguo nyekundu ambayo ni rangi ya chama hicho.

Aidha waandamanaji hao wamewataka wanajeshi waliotwaa madaraka ya nchi kuwaachilia huru viongozi inaowashikilia akiwemo Aung San Suu Kyi.

Tarehe Mosi ya mwezi huu wa Februari jeshi la Myanmar lilitangaza kudhibiti madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi nchini Myanmar, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo ambayo ilizua hofu ya kutokea mapinduzi.  

Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambap kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Malaysia Muhyiddin Yassin na Rais wa Indonesia Joko Widodo, wameelezea wasiwasi walio nao kuhusu mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar na kuwataka mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia kuandaa mkutano maalumu kuzungumzia suala la kudumisha uthabiti wa kisiasa katika eneo hilo.

342/