Main Title

source : parstoday
Jumatatu

15 Februari 2021

11:25:15
1115665

Majeshi ya Iran na Russia kufanya mazoezi makubwa ya kivita Bahari ya Hindi

Majeshi ya Majini ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia yatafanya mazoezi ya pamoja ya kivita kaskazini mwa Bahari ya Hindi. Hayo yamedokezwa na Admeri Habibullah Sayyari, Mratibu Mkuu wa Majeshi ya Iran ambaye ameongeza kuwa: "Kufanyika mazoezi hayo ni dhihirisho la nguvu za Majeshi ya Iran."

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran, Admeri Sayyari amesema hayo yatakuwa mazoezi ya pili ya pamoja ya kivita baina ya majeshi ya majini ya Iran na Russia na kuongeza kuwa: "Wakati Jeshi la Majini la nchi yenye uwezo mkubwa kama Russia linafanya mazoezi ya pamoja na Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, basi mazoezi kama hayo yanakuwa na ujumbe ulio wazi."

Mratibu Mkuu wa Majeshi ya Iran ameongeza kuwa, hii leo Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linaweza kulinganishwa na majeshi ya majini ya madola makubwa duniani kutokana na uwezo wake wa nguvu kazi, zana za kisasa na mbinu za kivita.

Admeri Sayyari amesema mazoezi hayo ya pamoja ya kivita ya Iran na Russia yanalenga kudumisha amani na usalama katika eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi.

Mratibu Mkuu wa Majeshi ya Iran ameashiria vitisho mbalimbali ambavyo Iran imekabiliana navyo kwa muda wa miaka 42 tokea baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema maadui wametekeleza njama mbalimbali lakini njama zao zimegonga mwamba.

Ameendelea kusema kuwa, sababu ya kushindwa maadui ni nguvu na uwezo wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

342/