Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

26 Mei 2022

12:11:37
1261190

Rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh, kuburuzwa mahakamani karibuni hivi

Serikali ya Gambia imekubaliana na mapendekezo yaliyotolewa na tume ya ukweli na maelewano iliyopendekeza rais wa zamani wa nchi hiyio, Yahya Jammeh apandishwe kizimbari kwa tuhuma za mauaji na utesaji watu wakati wa utawala wake.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Mwanasheria Mkuu wa Gambia, Dawda Jallow amesema kuwa, mahakama maalumu inapaswa kuundwa kwa ajili ya kufuatilia kesi za udhalilishaji zilizoripotiwa wakati wa utawala wa Jammeh wa kuanzia mwaka 1994 hadi 2017. Malalamiko hayo yamekabidhiwa kwa Tume ya Ukweli, Maelewano na Fidia (TRRC) iliyoundwa nchini humo baada ya kung'olewa utawala wa Jammeh.

Tume hiyo huru imesema kuwa, Jammeh na watu wake wanahusika na matukio 44 ya uhalifu dhidi ya waandishi wa habari, dhidi ya wanajeshi wa zamani, wapinzani wao wa kisiasa na raia wa kawaida zikiwemo kesi za mauaji na ubakaji.

Yahya Jammeh alitwaa madaraka ya nchi hiyo ndogo ya magharibi mwa Afrika mwaka 1994 kwenye mapinduzi ya kijeshi. Alilazimishwa kutoka madarakani mwaka 2016 licha ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais wa hivi sasa wa Senegal, Adama Barrow. Hivi sasa Jammeh anaishi ukimbizini Equatorial Guinea na amekuwa akikanusha madai yote yanayotolewa dhidi yake na serikali ya hivi sasa ya Rais Adama Barrow.

Akitangaza hadharani majibu ya serikali ya Senegal kwa ombi la tume ya TRRC, Mwanasheria Mkuu wa Gambia, Dawda Jallow amesema, kuna haja ya kuainishwa wakati maalumu na taratibu zilizo wazi kwa ajili ya utekelezaji wa pendekezo hilo la tume ya Tume ya Ukweli, Maelewano na Fidia (TRRC).

342/