Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

30 Mei 2022

13:50:23
1262314

Licha ya kuonesha uadui mkubwa, Ulaya yaendelea kutumia gesi ya Russia kupitia Ukraine

Licha ya kwamba nchi za Ulaya zinaendelea kuchukua hatua kali za kiuadui dhidi ya Russia na kuzilazimisha nchi nyingine kufuata siasa zao dhidi ya Moscow, lakini nchi hizo za Ulaya zimeshindwa kuacha kutumia gesi ya Russia.

Shirika la gesi la Russia, Gazprom, limesema kuwa, linaendelea kuziuzia gesi nchi za Ulaya kupitia bomba linalopitia Ukraine. Gazprom lilitoa taarifa hiyo jana Jumapili na kuongeza kuwa, si tu nchi za Ulaya hazijaacha kutumia gesi ya Russia, bali hata zimeongeza kiwango cha matumizi yao. Limesema, kiwango cha gesi ya Russia inayopelekwa kwa nchi za Ulaya kupitia Ukraine kimefikia mita-cubic milioni 44.1 wakati Jumamosi kiwango hicho kilikuwa ni mita-cubic milioni 43.96.

Tangu baada ya kuanza vita vya Ukraine tarehe 24 Februari mwaka huu hadi hivi sasa, nchi za Ulaya na za Magharibi kiujumla zinaendelea kuonesha uadui wa kupindukia dhidi ya Russia. Nchi hizo zimeiwekea Moscow vikwazo vikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo lakini pamoja na hayo, bado zinanunua kwa wingi nishati kutoka Russia ikiwemo gesi.

342/