Main Title

source : Parstoday
Jumatano

31 Agosti 2022

17:39:49
1302134

Waziri Mkuu wa Japan aahidi kufuatilia kiti cha Afrika katika Baraza la Usalama

Waziri Mkuu wa Japan amesema kuwa, nchi yake ina mpango wa kustafidi na nafasi na ushawishi wake katika Baraza la Usalama ili kuhakikisha kuwa, bara la Afrika linapatiwa kiti cha kudumu katika taasisi hiyo muhimu duniani.

Fumio Kishida, Waziri Mkuu wa Japan amesema hayo katika hotuba yake kwenye "Mkutano wa Kimataiifa wa Tokyo Kwa Ajili ya Ustawi wa Afrika" na kusisitiza kwamba, Japan imeazimia kufidia dhulma ya kihistoria dhidi ya bara la Afrika kutokana na bara hilo kutokuwa na mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri Mkuu huyo wa Japan amesema kuwa, ili Umoja wa Mataifa uwe na utendaji athirifu katika kuleta amani na suluhu duniani, kuna haja ya kufanyika mabadiliko ya haraka katika muundo wa Baraza la usalama la umoja huo.

Aidha Fumio Kishida amesema kuwa, Umoja wa Mataifa unakabiliwa na lahadha muhimu na zenye kuainisha hatima ya mambo.

Ikumbukwe kuwa, viongozi mbalimbali barani Afrika wamekuwa wakilalamikia dhulma katika muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na wamekuwa wakisisitiza kwamba, Afrika inapaswa kwa akali kuwa na mwanachama mmoja wa kudumu katika baraza hilo ambaye atakuwa na haki ya kura ya veto

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kishida ameahidi kwamba, Japan itatekeleza mipango ya uwekezaji wa kiwango cha dola bilionii 30 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Kadhalika amesema kuwa, Japan itamteua mjumbe wake maalumu katika masuala ya eneo la Pembe ya Afrika,342/