Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

23 Septemba 2022

18:17:59
1307516

Viongozi wa magharibi mwa Afrika wakubaliana kuiwekea Guinea vikwazo vya hatua kwa hatua

Viongozi wa nchi za magharibi mwa Afrika jana walikuwa na kikao cha dharura wamekutana pambizoni mwa Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifahuko New York, Marekani ambapo wamekubaliana kuiliwekea baraza la kijeshi la uongozi la Guinea vikwazo vya taratibu baada ya kushindwa kuainisha tarehe ya kurejea nchi hiyo katika utawala wa kiraia.

Kwa ufupi, kikao hicho dha dharura cha viongozi wa magharibi mwa Afrika huko New York kilifikia makubaliano kuhusu vikwazo vya taratibu kwa shakhsia wenye mfungamano na baraza la kijeshi linaloongoza Guinea ambao hivi karibuni watatajwa wazi na jumuiya ya Ecowas. 

Jumuiya ya Ecowas katika kipindi cha miaka miwili iliyopita  ikikabiliana na matukio mtawalia ya mapinduzi ya kijeshi katika ukanda huo. Mali ilikumbwa na mapinduzi ya kijeshi mara mbili mnamo Agosti mwaka juzi wa 2020 na mwezi Mei mwaka jana kisha ikafuatiwa na Guinea mwezi Septemba mwaka jana na Burkina Faso mwezi Januari.

Jumuiya ya Ecowas iliiondolea Mali baraza la kijeshi la nchi  hiyo baada ya kukubali kuainisha mwezi Machi mwaka 2024 kama tarehe ya kurejea nchi hiyo katika utawala wa kiraia. Pamoja na hayo lakini, Mali na Guinea zimezuiwa kushiriki katika taasisi za jumuiya ya Ecowas. 

342/