Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

29 Septemba 2022

20:17:08
1309092

Nusu ya Wamarekani wanapinga kutumwa silaha Ukraine

Uchunguzi mpya wa maoni umebaini kuwa, karibu nusu ya Wamarekani wanapinga kutuma misaada ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine.

Matokeo ya uchunguzi mpya wa taasisi ya Quincy Institute for Responsible Statecraft yanaonyesha kuwa, karibu nusu ya Wamarekani, (47%) wanapinga suala la kutumwa msaada wa kijeshi nchini Ukraine iwapo nchi yao haitashiriki katika juhudi za kidiplomasia za kutatua mgogoro huo. 

Utafiti huo pia uligundua kuwa asilimia 57 ya washiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni wanaunga mkono kuendelea kwa mazungumzo ya kidiplomasia ya Marekani ili kumaliza mgogoro wa Ukraine haraka iwezekanavyo, huku asilimia 32 pekee wakipinga juhudi hizo.

Wakati huo huo, wawakilishi wa Bunge la Marekani wanajaribu kutekeleza rasimu ya mpango wa msaada wa dola bilioni 12 kwa serikali ya Ukraine kutokana na ombi la Rais wa Marekani, Joe Biden.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken amesema "Ukraine inaweza kutumia silaha ilizopewa na Marekani kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya Russia, ambako kunafanyika kura ya maoni ya kujiunga na shirikisho la Urusi"

Nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujumla, hasa Marekani, zimezidisha mashinikizo ya vikwazo dhidi ya Russia ikiwa ni pamoja na kutuma kila aina ya silaha nyepesi na nzito kwa serikali ya Kiev, na hivyo kuchochea moto zaidi katika migogoro wa nchi hiyo.

342/