Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

1 Oktoba 2022

19:07:49
1309551

Putin atia saini mikataba ya kujiunga na Russia mikoa ya zamani ya Ukraine

Rais Vladimir Putin ametia saini mikataba ya kujumuisha mikoa minne ya zamani ya Ukraine katika Shirikisho la Russia. Sherehe ya Ijumaa iliashiria kuanza kwa mchakato rasmi wa mikoa hiyo kuwa sehemu ya Russia.

Wakuu wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk na Lugansk katika eneo la Donbass, Denis Pushilin na Leonid Pasechnik, pamoja na viongozi wa maeneo ya Kherson na Zaporozhye, Vladimir Saldo na Evgeny Balitsky, walitia saini hati hizo pamoja na Putin.

Hatua hiyo inafuatia maombi rasmi ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk na Lugansk pamoja na mikoa hiyo miwili ya kusini mwa Ukraine, ambayo ilikuwa imetangaza uhuru, kujiunga na Russia

Akizungumza baada ya hafla ya kutia saini mikataba hiyo, Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kujumuishwa kwa mikoa ya Donetsk, Lugansk, Kherson na Zaporozhye kunarekebisha dhuluma za kihistoria za ukoloni wa Magharibi. Aliongeza kuwa kwa kutambua hiari ya wakazi wa Donetsk, Lugansk, Kherson na Zaporozhye, Russia imewakumbatia watu wanaoshiriki historia na utamaduni wake na kurekebisha baadhi ya dhuluma zilizofanywa na Umoja wa Kisovieti.

Ameongeza kuwa Ukraine ilikusudia kuwakandamiza wazungumzaji wa Kirusi ndani ya mipaka yake na hivyo kuwafanya wakumbane na hatima ile ile ambayo wakoloni wa Magharibi wanataka kuitumia kueneza satwa yao ya kibeberu duniani.

Rais wa Russia amedokeza kuwa nchi za Magharibi zimekuwa zikisema kwa karne nyingi kwamba zinaleta uhuru na demokrasia kwa mataifa mengine katika hali ambayo madai hayo ni hadaa tupu. Amebaini kuwamba badala ya kuleta demokrasia wameeneza ukandamizaji na kuwapokonya watu uhuru na kuwafanya watumwa.

342/