Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

1 Oktoba 2022

19:08:35
1309552

Serikali za Ulaya zinaunga mkono rasmi chuki dhidi ya Uislamu

Mashirika ya kiraia ya Kiislamu yameshutumu nchi za Ulaya kwa kukandamiza jamii za Kiislamu, na hivyo kuzusha hali ya wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) inayofadhiliwa na serikali barani Ulaya.

Ufaransa, Denmark na Austria ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza sera ambazo wanaharakati wanasema zinachangia "kukandamiza kimfumo jumuiya za kiraia za Kiislamu". Akihutubia Kikao cha Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) huko Warsaw Alhamisi, Lamies Nassri, meneja wa mradi katika Kituo cha Haki za Waislamu (CEDA) nchini Denmark, amesema chuki dhidi ya  Uislamu inaenea kote Ulaya na kuzitaka serikali kulinda raia wao Waislamu.

Nassri amewaambia wajumbe: "Ni jukumu lenu kama nchi wanachama kuhakikisha kwamba raia katika nchi hizi wanachama wanalindwa dhidi ya ubaguzi wa rangi, ufuatiliaji, unyanyapaa na mashambulizi. Akiangazia hali nchini Denmark, Nassri amesema chuki dhidi ya Uislamu "inawezeshwa moja kwa moja kupitia sera ya serikali " na "si suala la mrengo mkali wa kulia bali linashirikiwa katika wigo wa kisiasa".

Nassri amesema Waislamu wengi nchini Denmark wanakabiliwa na ubaguzi kupitia kuainishwa kategoria ya wa watu kutoka asili zisizo za Magharibi ambao, amesema, wanaonekana kama raia wa daraja la pili ikilinganishwa na Wadenmark asili.

Wanaharakati kutoka Ufaransa wameangazia athari kwa jumuiya za Kiislamu za kile kinachoitwa "hati ya maimamu" ambayo ilipitishwa mwaka jana na Baraza la Imani ya Kiislamu la Ufaransa kwa amri ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Elias d'Imzalene wa shirika lisilo la kiserikali la Kifaransa Perspectives Musulmanes amesema hati hiyo inalenga kulazimisha "Uislamu mpya kwa mujibu wa matakwa ya serikali".

Mkutano huo pia ulimsikiliza Nehal Abdalla, ambaye alisema Polisi wa Austria wa kukabiliana na ugaidi walivamia makao ya familia 70 za Kiislamu na kuwakamata wasomi na wanaharakati 30 katika operesheni ya Novemba 2020, lakini hakuna hata mmoja aliyeshtakiwa kwa kosa lolote.

342/