Main Title

source : Parstoday
Jumapili

2 Oktoba 2022

19:52:13
1309935

Waislamu London walaani kuvunjiwa heshima thamani za Kiislamu

Waislamu wanaoishi London, mji mkuu wa Uingereza wamefanya maandamano ya kulalamikia vitendo vya kuvunjiwa heshima thamani za Kiislamu na chokochoko dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Waandamanaji hao ambao aghalabu yao walikuwa vijana, walikusanyika katika Kituo cha Kiislamu mjini London katika maandamano hayo ya kulaani kuvunjiwa heshima Matukufu ya Kiislamu.

Vijana hao wa Kiislamu mjini London walikuwa wamebeba bendera zenye jina la Imam Hussein (AS), mjukuu wa Tume Muhammad (SAW), na mabango yaliyokuwa na jumbe za kulaani wazusha fujo na maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Makundi hayo ya vijana yamesikika yakipiga nara za 'Hapana kwa idhilali' huku wakisisitiza kuwa, vitendo vya kuvunjia heshima Matukufu ya Kiislamu havipaswi kuvumiliwa.

Maandamano hayo ya jana mjini London yaliungwa mkono na akthari ya uongozi wa misikiti, vituo na jumuiya za Kiislamu nchini Uingereza.

Yamefanyika wiki moja baada ya kundi la watu wanaopinga Mapinduzi kukusanyika nje ya ubalozi wa Iran mjini London, na kuwashambuliwa waombolezaji wa Arubaini ya Imam Hussein (AS), mbali na kuwavua hijabu wanawake wa Kiislamu.

Polisi ya London imechapisha picha za watu 13 waliohusika na vurugu za wiki jana nje ya  ubalozi wa Iran mjini hapo, fujo ambazo zilizokosolewa vikali pia na Meya wa London.

342/