Main Title

source : Parstoday
Jumapili

2 Oktoba 2022

19:53:37
1309937

WHO yatahadhariasha: Kipindupindu kinaongezeka kote duniani

Shirika la Afya Duniani limeonya kwamba baada ya miaka ya kupungua, visa vya kipindupindu vinaongezeka ulimwenguni.

Shirika la Afya Duniani limesema ongezeko la wagonjwa wa kipindupindu ulimwenguni linatia wasiwasi mkubwa.

 Philippe Barboza, mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kipindupindu na kuhara cha WHO, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva kwamba, kumeshuhudiwa kasi ya ongezeko la ugonjwa wa kipindupindu na kwa kipimo kikubwa zaidi.

Kesi za maambukizi ya kipindupindu zimeripotiwa katika nchi zisizopungua 26 katika miezi tisa ya mwaka huu pekee.

Barboza amesema: Kuna wasiwasi mkubwa zaidi wa maambukizi ya kipindupindu huko kusini mwa Afrika, Bara Hindi, Afghanistan, Bangladesh, Pakistan, Nepal na nchi jirani, na hali hii inaweza kuenea katika nchi nyingine zilizoathirika kama vile Lebanon.

Kiwango cha vifo vinavyosababishwa na kipindupindu barani Afrika pia kimefikia asilimia 3, takwimu ambazo ni kubwa sana zikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kipindupindu na kuhara cha WHO anasema, athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kama mafuriko, tofani, ukame na kadhalika zimesababisha ukosefu wa maji safi na salama na kutayarisha mazingira ya kuibuka maradhi ya kipindupindu.  

342/