Main Title

source : Parstoday
Jumatano

5 Oktoba 2022

18:44:43
1310817

Waziri Mkuu wa Ufaransa: Russia itabaki kuwa dola kuu lenye nguvu

Waziri Mkuu wa Ufaransa Elizabeth Bourne amesema: Russia ilikuwa na itaendelea kuwa dola kuu lenye nguvu, na wala haitaweza kupuuzwa hata baada ya vita vya Ukraine.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Iran IRIB, Bourne amesema katika hotuba aliyotoa kwenye Baraza la Taifa la Ufaransa kuwa Russia itaendelea kuwa dola lenye nguvu ambalo haliwezi kupuuzwa, na akaongezea kwa kusema: operesheni za kijeshi nchini Ukraine zitaendelea kwa muda mrefu.Mbali na kutilia mkazo kuendelezwa vikwazo dhidi ya Russia, waziri mkuu wa Ufaransa amesema, nchi yake itaendelea kuiunga mkono Ukraine hadi pale nchi hiyo itakapoona ni wakati mwafaka kufanya mazungumzo na Moscow.Vita vya Ukraine vinaendelea kwa mwezi wa nane sasa licha ya athari zake kubwa na hasi za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kitamaduni; na wakati huohuo nchi za Magharibi zingali zinaendelea kuipelekea silaha Ukraine.Kwa hatua yao ya kushadidisha vikwazo dhidi ya Russia na kuipatia Ukraine anuai za silaha nyepesi na nzito, nchi za Ulaya na Magharibi, hasa Marekani, sio tu hazijapiga hatua yoyote kusaidia kukomesha vita vya Ukraine, lakini kwa hatua zao hizo, zinakoleza zaidi moto wa vita na mapigano katika nchi hiyo.../

342/