Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

6 Oktoba 2022

18:30:30
1311129

FBI: Watu 22,900 waliuawa Marekani mwaka 2021

Idadi ya mauaji yaliyoripotiwa nchini Marekani iliongezeka mwaka jana, huku idadi kubwa ya mauaji hayo yakifanywa kwa kutumia aina fulani ya bunduki.

Kulingana na ripoti mpya ya Idara ya Upelelezi ya Marekani, FBI, mauaji yaliyoripotiwa nchini Marekani yaliyongezeka kwa 4.3% mwaka jana ikilingnaishwa na mwaka 2020.

Kulingana na ripoti hiyo mpya, idadi ya mauaji iliongezeka kutoka 22,000 mnamo 2020 hadi 22,900 mnamo 2021.

Maafisa, hata hivyo, walionya kuwa takwimu za FBI hazijakamilika na zilitenga baadhi ya miji mikubwa, kama New York na Los Angeles, kutokana na mfumo mpya wa kufuatilia data.

"Uhalifu wa kikatili umeongezeka katika nchi hii chini ya utawala wa Biden," Mwakilishi wa chama cha Republican Michael Burgess wa Texas amesema katika taarifa, akibainisha ripoti mpya ya FBI kuhusu mauaji inaibua wasiwasi mkubwa.

Takwimu mpya pia zilionyesha kuwa asilimia 58 ya wahasiriwa wa mauaji walikuwa watu weusi, asilimia 37 wazungu na asilimia 14 walatino.

342/