Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

6 Oktoba 2022

18:33:41
1311136

Iran: Tutatoa jibu iwapo EU itaendelea na tabia yake ya uingiliajii

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametahadharisha kuwa, Tehran itatoa jibu mwafaka iwapo Umoja wa Ulaya utaendelea na tabia yake ya kungilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu.

Hossein Amir-Abdollahian alitoa indhari hiyo jana Jumatano katika mazungumzo yake ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia,  Luigi Di Maio na kueleza kuwa, "Iwapo EU inataka kuchukua hatua ghalati na iliyoharakishwa (dhidi ya Iran), basi isubiri jibu athirifu la Iran."

Ameashiria haki ya kufanya maandamano hapa nchini na kueleza bayana kuwa, "Kwa mara nyingine tena, wananchi shupavu wa Iran, huku wakiwa na muono wa mbali wa kisiasa, hawajaruhusu uingiliaji wa kigeni, na kudhuriwa uhuru wa kisiasa na mamlaka ya kujitawala nchi hii."

Haya yanajiri wakati huu ambapo Umoja wa Ulaya umesema kuwa unatafakari suala la kuiwekea Iran vikwazo, eti kutokana na kifo cha binti Muirani Mahsa Amini, na kukandamizwa maandamano ya kulaani kifo hicho.

Wawili hao pia wamejadili uhusiano wa pande mbili wa Iran na Italia, masuala ya kieneo na kimataifa, na kadhia ya kuondolewa Iran vikwazo vya kidhalimu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia,  Luigi Di Maio amesema nchi yake itaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa makubaliano ya kuondolewa Iran vikwazo yanafikiwa karibuni.

342/