Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

6 Oktoba 2022

18:34:12
1311137

Makumi wauawa katika mripuko mwingine wa bomu msikitini Kabul

Makumi ya watu wamepoteza maisha katika shambulio la bomu lililolenga msikiti mmoja huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, kwenye ua wa Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya Taliban.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya al-Jazeera, watu 25 wameaga dunia kwenye mripuko huo wa jana Jumatano, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa.

Abdul Nafy Takor, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya Taliban amesema mripuko huo ulijiri wakati  maafisa wa wizara hiyo na wageni wengine walikuwa wakiswala Swala wa Alasiri.

Amesema watu 4 wameuawa huku 25 wakijeruhiwa. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa, na hadi sasa hakuna mtu au kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo.

Mripuko huo umetokea siku chache baada ya hujuma nyingine ya kigaidi ya Ijumaa iliyopita iliyolenga kituo cha elimu, kuua watu 53 wakiwemo wanawake na wasichana 46 waliokuwa wanafanya mtihani wa kuingia chuo kikuu. 

Katika miezi na wiki zilizopita, Afghanistan imeshuhudia miripuko na mashambulizi ya kigaidi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Kabul yaliyolenga misikiti ya Mazar-e-Sharif na Kunduz ambayo yamesababisha mamia ya watu kuuawa na kujeruhiwa.

Kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) limekiri kuhusika na mashambulio mengi miongoni mwa hayo. Serikali ya mpito ya Taliban haijaweza kudhamini usalama unaohitajika katika mji wa Kabul na miji mingine ya nchi hiyo.

342/