Main Title

source : Parstoday
Jumanne

18 Oktoba 2022

16:24:29
1314989

Wakongomani wataka Umoja wa Mataifa utangaze mauaji ya mara kwa mara ya DRC kuwa ya kimbari

Wakazi wa Beni, Kivu kaskazini, na Ituri wanaiomba serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Umoja wa Matifa kutangaza mauaji ya mara kwa mara katika maeneo hayo kuwa ya kimbari.

Akizungumza na wanahabari akiwa katika eneo la makaburi ya watu 33 waliouawa kwa mapanga na visu mwaka 2014 Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni wakati wa kuadhimisha miaka minane tangu yaanze mauaji katikatika mwa mji wa Beni, Rachel Muvunga, mmoja wa wakaazi wa Beni ambao wamepoteza wanafamilia wao, ameitaka serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kutangaza rasmi mauaji dhidi ya raia wa Beni, Lubero na hata Ituri kuwa ni ya kimbari akisema kwamba kila uchao, watu huuawa kwa mapanga na shoka wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Muvunga ambaye amekuwa mwanaharakati kwa zaidi ya miaka thelathini aliomba wananchi pamoja na serikali kushikamana wakati huu mgumu wa mauaji ya kila siku.

Katika upande mwingine serikali ya Kinshasa kujenga mnara mjini Beni kama alama ya kihistoria ili mauaji ya Beni yatambulikane kimataifa na kwa vizazi vijavyo.

342/