Main Title

source : Parstoday
Jumatano

26 Oktoba 2022

17:53:52
1317487

Serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray waanza mazungumzo ya amani, Johannesburg

Rais wa Afrika Kusini amesema kuwa mazungumzo ya amani kati ya wawakilishi wa serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray huko kaskazini mwa nchi hiyo, yamenza katika mji wa Johannesburg.

Hapo awali, Umoja wa Afrika ulikuwa umetoa wito wa kusitishwa mara moja na bila masharti uhasama na mapigano kati ya kundi la Tigrayan People's Liberation Front (TPLF),  na vikosi vya jeshi la Ethiopia.

Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini imetangaza kuwa mazungumzo rasmi kati ya wawakilishi wa serikali ya Ethiopia na Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray (TPLF) yalianza jana Jumanne mjini Johannesburg na yataendelea hadi Jumapili ijayo.

Ujumbe wa waasi wa Tigray umetangaza kuwa, mazungumzo ya Afrika Kusini yamejikita katika suala la kusitishwa uhasama, utoaji wa huduma kwa wakazi wa Tigray na kurudi nyuma vikosi vya jeshi la Eritrea. Serikali ya Ethiopia pia imetangaza kuwa mazungumzo hayo ni fursa ya kutatua mgogoro huo na kuboresha hali ya watu wa Tigray.

Eritrea inaisadia serikali ya Ethiopia katika mashambulizi yake dhidi ya waasi wa Tigray.

Mazungumzo hayo ya amani yalitazamiwa kusimamiwa na mjumbe wa Umoja wa Afrika, Olusegun Obasanjo, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Phumzile Mlambo-Ngcuka na rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Machafuko na vita vinavyoshuhudiwa katika eneo la Tigray huko kaskazini mwa Ethiopia vimepelekea kuuliwa makumi ya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

342/