Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

28 Oktoba 2022

19:27:19
1318107

Umoja wa Mataifa wasisitiza dhamira yake ya kusitisha vita nchini Libya

Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kwa mara nyingine amesisitiza dhamira ya taasisi hiyo ya kimataifa ya kusitisha vita nchini humo.

Abdoulaye Bathily, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres nchini Libya, ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba, chombo hicho cha kimataifa kinasisitiza dhamira yake ya kuunga mkono juhudi za kusitisha vita nchini Libya kupitia Kamati ya Pamoja ya Kijeshi ambayo ilipanga kufanya mkutano jana Alhamisi katika mji wa Sirte, katikati mwa Libya.

Abdoulaye Bathily pia amesisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kutoa msaada wa kiufundi kwa Kamati ya Pamoja ya Kijeshi ya Libya ili kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano nchini humo.

Mgogoro wa kisiasa nchini Libya unaongezeka kila uchao kutokana na hitilafu zilizopo kati ya serikali hizo mbili zinazotawala nchi hiyo.

Mwaka 2011, nchi wanachama wa shirika la kijeshi la NATO zilifanya mashambulizi makubwa dhidi ya Libya kwa kisingizio cha kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi. Baada ya kupinduliwa Gaddafi, Libya iliingia katika kipindi cha machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo vingali vinaendelea na hadi sasa nchi hiyo haijaweza kushuhudia amani na utulivu.

342/