Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

28 Oktoba 2022

19:29:18
1318111

UN yasema haijui fedha chungu nzima za misaada ya Afrika, zimeishia wapi

Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, umoja huo haujui fedha chungu nzima zilizotengwa kwa ajili ya nchi za Afrika, ziko wapi na ziko mikononi mwa nani.

Shirika la habari la Sputnik limemnukuu Martin Griffiths, Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa akizungumzia dola bilioni mia moja za umoja huo kwa ajili ya kupambana na ukame na umaskini barani Afrika na kusema kuwa, hivi sasa tumo katika harakati za kutafuta kujua fedha za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika na ambazo Umoja wa Mataifa uliahidi kuzitoa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, sasa hivi ziko wapi? Ziko mikononi mwa nani na ni nani anayehusika na kutofika fedha hizo kwa nchi za Afrika kama Somalia? 

Afisa huyo wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa pia amesema, wananchi wa Somalia ni wahanga wa vitendo na tabia zetu. Hadi hivi sasa tumeshindwa kuwafikishia fedha ambazo tuliwaahidi miaka mingi nyuma.

Vile vile amesema, wakati alipoyauliza mataifa mbalimbali kuhusu namna ya kudhamini fedha na kuzigawa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hakupata majibu kutoka kwa serikali yoyote. 

Kwa miaka mingi sasa Somalia inateseka kwa janga la ukame na ukosefu wa mvua mbali na machafuko ya ndani na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalliyochukua muda mrefu bila ya kuweko matumaini ya kutatuliwa.

342/