Main Title

source : Parstoday
Jumapili

30 Oktoba 2022

19:30:13
1318873

Watu 100 wauawa, mamia wajeruhiwa katika mripuko wa magari mawili Somalia

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, ametangza kuwa watu 100 wameuawa na wengine 300 wamejeruhiwa katika mlipuko wa magari mawili yaliyokuwa yametengwa mabomu mjini Mogadishu.

Awali Wizara ya Afya ya Somalia ilikuwa imetangaza kuwa idadi ya watu waliouawa katika mlipuko wa alasiri ya jana kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu imefikia 50.

Duru mbalimbali za habari zimeripoti kutokea mripuko wa magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na kuua watu wasiopungua 50 na kujerumi makumi ya wengine.

Televisheni ya Al Jazeera ya Qatar ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoripoti habari hiyo na kusema kuwa, kumesikika sauti ya kutisha wakati wa mripuko huo ulipotokea. Mwandishi wa televisheni hiyo mjini Mogadishu amesema, sambamba na mripuko huo, kumesikika pia sauti za risasi katika makutano ya barabara tatu mjini humo. Mripuko huo umelenga Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu mjini Mogadishu.

Awali shirika la habari la Ujerumani lililinukuu jeshi la polisi la Somalia likisema kuwa, watu wasiopungua 10 wameuawa katika shambulio hilo la kigaidi. Mripuko huo umetokea zikiwa zimepita siku chache tangu vyombo vya intelejensia vya Somalia vikishirikiana na vya kimataifa kuangamiza wanachama 17 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari ya Somalia, magaidi hao waliuawa katika operesheni ya usiku wa kuamkia Jumatano ya tarehe 26 Oktoba katika mji wa Hawadley, ulioko umbali wa takriban kilomita 40 kaskazini mwa Mogadishu.

Taarifa ya wizara hiyo ilisema, operesheni hiyo ilifanywa na Idara ya Taifa ya Intelijensia kwa kushirikiana na washirika wa kimataifa na kuongeza kuwa, wanachama hao wa al-Shabaab walishambuliwa walipokuwa wamekusanyika katika eneo moja mjini Hawadley na kuangamizwa 17 miongoni mwao. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, raia 1,242 wameuawa katika mashambulizi ya kigaidi nchini Somalia baina ya mwaka 2018 na 2019 na wengine zaidi ya 1,735 wamejeruhiwa katika kipindi cha baina ya miaka hiyo.

342/