Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

31 Oktoba 2022

19:49:43
1319249

Hitilafu za mpaka zashtadi kati ya Algeria na Morocco

Kuchapishwa ramani ya Ulimwengu wa Kiarabu inayoonyesha mstari unaoigawa Sahara Magharibi kumeibua malalamiko na kukosolewa na Morocco na kupelekea ujumbe wa nchi hiyo kuondoka katika kikao cha faragha cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League).

Kwa kuzingatia hitilafu zilizopo za mpaka kati ya Algeria na Morocco, hatua ya kuchapishwa ramani hiyo ya Ulimwengu wa Kiarabu inayoonyesha mstari unaoigawa sahaha Magharibi imeibua mvutano wa kisiasa kati ya nchi za Kiarabu ikiwa ni katika kukaribia kufanyika mkuktano wa wakuu wa nchi za Kiarabu huko Algeria.  

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Arab League walikuwa wameitisha kikao chao cha faragha kwa ajili ya kuainisha ajenda ya kazi ya mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliopangwa kufanyika Jumanne na Jumatano wiki hii huko Algeria.  

Kituo cha habari cha EL 24 News cha Algeria ndicho kilichochapisha ramani hiyo tajwa ya Ulimwengu wa Kiarabu, hata hivyo kimeomba radhi katika ukurasa wake wa Facebook baada ya kuibuka makelele na kueleza kuwa: kuchapishwa ramani hiyo lilikuwa kosa la mtu binafsi na la kiufundi.

Baada ya kuibuka malalamiko na ukosoaji dhidi ya kuchapishwa ramani hiyo ya Ulimwengu wa Kiarabu inayoonyesha mstari unaoigawa sahaha Magharibi nayo Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetangaza kuwa,  utangazaji wa shughuli za mkutano huo hauna mshirika yoyote wa vyombo vya habari na hakuna ramani yoyote rasmi inayoonyesha mipaka ya kisiasa kati ya nchi za Kiarabu; na kwamba inathibitisha na kutumia ramani ya Ulimwengu wa Kiarabu bila ya mipaka kati ya nchi za ulimwengu huo kwa ajili ya kuimarisha fikra ya Umoja wa Kiarabu. 

Mkutano wa wakuu wa Arab League umepangwa kufanyika huku viongozi wa nchi sita wakitangaza kutohudhuria; suala ambalo limeibua shaka iwapo mkutano huo utazaa matunda au la.  

342/