Main Title

source : Parstoday
Jumanne

8 Novemba 2022

18:26:39
1321403

Afisa wa jeshi la Marekani: Karibuni hivi tutaingia kwenye mapigano ya muda mrefu na China

Afisa mwandamizi wa jeshi la Marekani amesema karibuni hivi nchi hiyo itaingia kwenye mzozo na makabiliano ya muda mrefu na China na akatahadharisha juu ya kile alichoeleza kuwa ni kubaki nyuma Washington katika uwezo wa kijeshi mkabala na Beijing.

Adimeri Charles Richard, mkuu wa Kamandi ya Kimkakati ya Jeshi la Wanamaji la Marekani, ametahadharisha kuwa, karibuni hivi nchi hiyo itaingia kwenye mzozo na mapigano ya muda mrefu na China, na kwamba makabiliano hayo yatakuwa tofauti na iliyokabiliana nayo Washington huko nyuma. Kwa mujibu wa shirikia la habari la Sputnik, Richard amesema katika Kongamano la jeshi la Wanamaji la Marekani: "tunahitaji kufanya mabadiliko ya haraka na ya kimsingi katika mbinu zetu za kiulinzi. Mgogoro wa Ukraine tuliomo ndani yake hivi sasa ni njia ya maandalizi makubwa tu, na muda si mrefu tutakabiliana na hatua mpya za vita ambazo hatukuwahi kukumbana nazo hapo kabla."

Mkuu huyo wa kamandi ya kistratejia ya jeshi la wanamaji la Marekani ameashiria hali hatarishi inayokabiliana nayo Washington na akaonya kwa kusema, meli inazama polepole, kwa sababu China inaonyesha uwezo mpya wa kijeshi kwa kasi zaidi kuliko Marekani, na kutokana na hali hiyo karibuni hivi Wachina watakuwa na uwezo mkubwa zaidi katika medani ya mapigano.

 Afisa huyo mwandamizi wa jeshi la Marekani amekosoa pia kuzorota kwa mfumo wa kijeshi wa Marekani na akasema, ustadi mkuu unaotakikana ni kuweza kutoa mifumo mipya na kwa haraka, si kubaki nyuma kimaendeleo katika mabadiliko yanayojiri hivi sasa! Adimeri Richard ameendelea kueleza kuwa Marekani hivi sasa imepitwa na China katika uga wa makombora; na kwamba China inatumia kizazi cha makombora ya cruise yanayofika masafa ya mbali mno, majimui ya anuai za makombora ya balestiki na aina kadhaa za silaha zenye kasi kubwa zaidi ya sauti ambazo Marekani haiwezi kukabiliana nazo kwa namna yoyote ile. Kwa mujibu wa afisa huyo wa Marekani, Beijing ina rada yenye uwezo wa kubaini ndege zinazokwepa kunaswa na rada na imejizatiti kwa manowari za kisasa kabisa ambazo ni tishio na hatarishi kwa meli za kivita za Washington za F-22 na F-35.../


342/