Main Title

source : Parstoday
Jumanne

8 Novemba 2022

18:29:00
1321407

Iran: Tutapambana vilivyo na magaidi wote wanaohatarisha usalama wetu

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), amewatembelea hospitalini maafisa wa polisi waliojeruhiwa katika machafuko ya hivi karibuni humu nchini na kusisisitiza kuwa Tehran itapambana vilivyo na magaidi wanaohatarisha usalama wa nchi.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu Mohammad Bagher Ghalibaf akisema hayo katika Hospitali ya Vali Asr hapa Tehran wakati alipokwenda kuwajulia hali maafisa wa polisi waliojeruhiwa na wafanyaghasia humu nchini. 

Aidha ameelezea nafasi muhimu sana ya jeshi la polisi katika kulinda usalama na kudumisha amani ya nchi na kuongeza kuwa, baadhi ya wahalifu wametumia vibaya malalamiko ya wananchi kuanzisha fujo na kuharibu mali za umma na za wananchi wa kawaida pamoja na kufanya mauaji, uporaji na wizi. 

Magaidi walivamia haram tukufu ya Shah Cheragh mjini Shiraz na kufanya jinai kubwa

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza pia kuwa, hivi sasa imezidi kuonekana wazi jinsi adui alivyopanga njama kubwa za kuharibu mali za umma, kuendesha vitendo vya kigaidi na kuua wananchi na maafisa usalama ndani ya Iran.

Katika machafuko ya hivi karibuni humu nchini, viongozi wa kisiasa wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya pamoja na vyombo vyao vya habari zikiwemo televisheni za lugha ya Kifarsi zilizopewa uwanja wa kuendesha propaganda katika ardhi ya Uingereza kama BBC Persia, Manoto na televisheni ya Saudia ya Iran International, hawakupuuza fursa yoyote ya kuchochea machafuko, kujaribu kuigawa vipandevipande Iran, mauaji na uharibufu wa mali za umma na za watu wa kawaida humu nchini. 

Wananchi wa Iran lakini wamepevuka kisiasa na wamejitokeza kwa mamilioni kwenye maandamano ya siku na nyakati tofauti katika kona zote za nchi, kuvunja njama hizo za maadui.

342/