Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:19:19
1321762

Aliyemrushia mayai Mfalme Charles kupinga utawala wa kifalme Uingereza, atiwa nguvuni

Vyanzo vya habari vya Uingereza vimeripoti leo Jumatano kukamatwa kwa mwanamume aliyemrushia mayai Mfalme Charles III na mkewe, Camelia, wakati wa ziara yakke eneo la York.

Raia huyo alimrushia mayai Mfalme Charles III akipinga utawala wa kifalme chini Uingereza.

Picha zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari vya Uingereza zinawaonyesha maafisa wa polisi wakimvamia mshambuliaji na kumtoa nje ya umati.

Duru za habari zimefichua kuwa, mayai matatu yalitupwa kwa mfalme wa Uingereza, lakini hakuna hata moja lililompiga yeye au mke wake.

Charles alirithi kiti cha utawala wa kifalme wa Uingereza baada ya kifo cha mama yake, Elizabeth II Septemba mwaka.

Mfalme Charles ameshambuliwa mara kadhaa na wapinzani wa mfumo wa kifalme katika nchi hiyo.

Wakati wa mazishi ya Malikia Elizabeth, ambayo inakadiriwa kwamba yamegharimu mabilioni kadhaa ya pauni za walipakodi, baadhi ya waandamanaji walisema kwamba ubadhirifu wa familia ya kifalme unafadhiliwa kwa fedha ya raia wanaosumbuliwa na gharama za maisha.

Hali ya uchumi wa Uingereza inaripotiwa kuwa mbaya zaidi hivi sasa ikilinganishwa na kipindi cha nusu karne iliyopita kutokana na migogoro kadhaa mtawalia inayoisumbua nchi hiyo.

342/