Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:19:57
1321763

Uchunguzi: Wamarekani wingi weusi hawawezi kushiriki katika chaguzi za Marekani

Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa idadi isiyo na kikomo ya raia weusi wa Marekani hawawezi kushiriki katika chaguzi zinazofanyika chini humo.

Utafiti wa hivi karibuni zaidi wa taasisi ya "The Sentencing Project" unaonyesha kuwa asilimia 21 ya raia weusi katika jimbo la Tennessee huko Marekani hawawezi kupiga kura katika chaguzi za nchi hiyo.

Licha ya juhudi za kutaka kurekebisha tatizo hilo huko Tennessee ili kuwawezesha Wamarekani weusi kupiga kura, lakini kutokana na sera za ubaguzi wa rangi, inaoneka kuwa suala hilo litakuwa gumu kwa sababu Warepublican hawataweza kupata idadi kubwa ya kura za watu weusi.

Uchaguzi wa katikati ya muhula ulifanyika nchini Marekani jana Jumanne, ambapo viti vyote 435 vya Baraza la Wawakilishi na 35 kati ya 100 vya Seneti vimegombewa. 

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Warepublican wanaelekea kupata uushhindi na kulidhibiti Baraza la Wawakilishi kutoka kwa Democrats katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa Congress ya Marekani, ingawa uwezekano wa kupata ushindi wa kishindo unaonekana kuwa mdogo. 

Sambamba na uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani, wasiwasi umeongezeka zaidi kuhusu uwezekano wa kutokea ghasia za kisiasa na vitisho dhidi ya demokrasia katika nchi ambayo inadai kuwa kinara wa demokrasia duniani.

Matokeo ya uchunguzi mpya uliofanywa na ABC News na Washington Post yanaonyesha kuwa karibu Wamarekani 9 kati ya 10, sawa na asilimia 88, wana wasiwasi kwamba kukithiri kwa tofauti za kisiasa kunazidiasha hatari ya ghasia zinazochochewa na siasa nchini Marekani. 

Itakumbukwa kuwa Wamarekani wasiopungua 6 waliuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020. 

342/