Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:20:34
1321764

Russia: Bado hatujaafiki rasmi kurefusha usafirishaji nje wa nafaka za Ukraine

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, Moscow bado haijaamua rasmi kuafiki kurefushwa usafirishaji nje wa nafaka za Ukraine.

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la FARS ambalo limenukuu Andri Rudenko akisema hayo jana na kuongeza kuwa, Russia ndio kwanza inafikiria iwapo iafiki kurefushwa usafirishaji nje nafaka za Ukraine au la kutokana na kuwa uzoefu wa huko nyuma unaonesha kwamba nafaka hizo hazizifikii nchi maskini na zenye mahitaji. Vile vile ameulaumu Umoja wa Mataifa kwa kutotekeleza majukumu yake wakati ndicho chombo kikuu cha kutatua masuala ya kimataifa.

Amesisitiza pia kuwa, Moscow haioni maendeleo yoyote kutoka kwa nchi za Magharibi kuhusu mbolea na vyakula vinavyozalishwa Russia. 

Wiki moja nyuma serikali ya Shirikisho la Russia ilitangaza kuwa, imeafiki kuanza kusafirishwa tena nje nafaka za Ukraine baada ya kusimama kwa siku kadhaa.

Jumatano ya wiki iliyopita, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza kuwa, imepata dhamana inayotakiwa kutoka kwa Ukraine kuhusu kusafirishwa nje bidhaa za nchi hiyo. Wizara hiyo ilisema, Ukraine imetoa dhamana ya maandishi chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Uturuki.

Hata hivyo inaonekana viongozi wa Russia wameona kuwa bidhaa hizo hazizifikii nchi zenye mahitaji bali zinaishia kwa nchi za Magharibi ambazo zinaendesha vita vya pande zote dhidi ya Russia kwa mgongo wa Ukraine.

342/