Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:22:51
1321768

Raisi: Ushirikiano wa nchi huru ndio jibu kwa mkakati wa Marekani wa kudhoofisha usalama

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ushirikiano wa nchi huru ndilo jibu muhimu zaidi kwa stratijia ya Marekani ya kuyumbisha usalama.

Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo katika mazungumzo yake na Katibu wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Russia aliyeko safarini hapa nchini Iran.

Kikao hicho kimesisitiza udharura wa kupanuliwa zaidi ushirikiano wa kistratijia na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili na kuelezwa kuwa, kuimarisha ushirikiano wa kieneo ndio njia bora zaidi ya kuimarisha amani na utulivu.

Katika mazungumzo yake na Katibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia, Nikolai Patrushev, Sayyid Ebrahim Raisi ameeleza kuwa, irada na azma ya Iran na Russia ni kuinua kiwango cha uhusiano wa kistratijia katika nyanja mbalimbali na kusema: Ushirikiano wa nchi huru ndio jibu madhubuti zaidi kwa vikwazo na sera ya kuvuruga utulivu ya Marekani na washirika wake.

Akisisitiza kuwa siasa za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kupinga vita, Raisi ameongeza kuwa: Kupanuka na kushadidi vita ni jambo linalozitia wasiwasi nchi zote.

Katibu wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Russia pia aliwasilisha ripoti kuhusu hali ya ushirikiano wa pande mbili na kusisitiza kuwa: "Tunafanya kazi kwa bidii ili kuendeleza ushirikiano katika nyanja za siasa, biashara, nishati, kilimo na usafirishaji baina ya Iran na Russia. Amesema Tume ya Uchumi pia inafuatilia utekelezaji wa mikataba iliyotiwa saini na Marais wa nchi mbili.

Nikolai Patrushev ameelezea matumaini ya kustawishwa zaidi uhusiano wa Russia na Jamhuri ya Kiislamu katika mfumo wa mabaraza na asasi za kikanda na kusema: Kuwepo ulimwengu wa pande kadhaa kunakwenda sambamba na maslahi ya nchi zote duniani.

342/