Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:24:52
1321771

EAC yasisitiza kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa Kongo

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamekubaliana katika kikao kilichofanyika Cairo, Misri kwamba mgogoro wa mashariki mwa Kongo unapasa kutatuliwa kwa njia za kiraia na kupitia mazungumzo.

Maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameathiriwa na ukosefu wa amani tangu miaka 20 iliyopita ambapo mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi wenye silaha yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara.  

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jana walikutana pambizoni mwa Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi huko Sharm Sheikh, Misri. ambapo walijadili hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  

Rais Evariste Ndayishimiye Rais wa Burundi na Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Paul Kagame wa Rwanda, William Ruto wa Kenya, Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jean-Michel Sama Lukonde wamekubalina katika kikao hicho juu ya kuupatia ufumbuzi mzozo wa mashariki mwa Kongo kwa njia za amani.

Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamesisitiza katika taarifa yao ya pamoja kuwa, ufumbuzi wa kisiasa ndio njia pekee endelevu kwa ajili ya kurejesha amani na usalama mashariki mwa Kongo. 

Hii ni katika hali ambayo, siku moja baada ya viongozi wa EAC kuafikiana kuhusu kusitishwa mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kumeripotiwa ongezeko la mapigano kati ya waasi wa kundi la M23 na jeshi la Kongo ambalo limewalazimisha maelfu ya wakazi wa mashariki mwa nchi hiyo kukimbilia nchi jirani ya Uganda.  

Kongo na mzozo wa waasi wa M23Kenya, Uganda na Burundi zimeahidi kupeleka wanajeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati huo huo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekataa Rwanda kutuma wanajeshi wake katika ardhi ya nchi hiyo. 


342/