Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:25:30
1321772

Marandi: Matamshi ya Biden dhidi ya Iran ni juhudi za mfa maji

Mshauri wa timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran amejibu matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Marekani akiigilia kati masuala ya ndani na matukio ya hivi karibuni nchini Iran, na ameyataja matamshi hayo kuwa ni "juhudi za mfa maji".

Sayyid Mohammad Marandi, mshauri wa timu ya Iran katika mazungumzo ya Vienna, ameandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba: "Jaribio lisilo na tija la hivi majuzi la kutaka kuiyumbisha Iran lilikuwa pumzi za mwisho la ufalme unaoelekea kutoweka, ambao unazama katika migogoro ya nje na migawanyiko ya ndani."

Itakumbukwa kuwa siku chache zilizopita Rais wa Marekani Joe Biden alisema kwenye mkusanyiko wa kampeni za uchaguzi huko California kwamba: "Tutaikomboa Iran".

Matamshi hayo ya kibeberu ya Rais Joe Biden wa Marekani aliyeunga mkono ghasia na machafuko nchini Iran, yalijibiwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu, Sayyid Ebrahim Raisi,  ambaye alisema: "Inaonekana Biden ametoa matamshi hayo kutokana na hali yake ya kupoteza uelewa na umakini. Anapaswa kuelewa kwamba Iran ilikombolewa miaka 43 iliyopita na haitatekwa tena na Marekani wala kuwa gombe la kukamuliwa maziwa."

Vilevile Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran alijibu matamshi ya Joe Biden ya kuingilia masula ya ndani ya Iran kati katika ujumbe wake wa Twitter. Ameashiria sera za Marekani za kuzusha ghasia na kuchochea machafuko ya hivi karibuni katika baadhi ya miji ya Iran na kumwambia Biden kwamba: "Acha tabia ya unafiki na sitisha uungaji mkono kwa kundi la kigaidi la Daesh." 

342/