Maria Zakharova, ameeleza hayo katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari ambao umefanyika kwa njia ya intaneti na akaongeza kwa kusema: "tuko tayari kufanya mazungumzo na Ukraine kulingana na hali halisi ya sasa".Kuhusu matamshi yaliyotolewa na viongozi wa Ujerumani kwamba Russia haiko tayari kufanya mazungumzo na Ukraine, Zakharova amesisitiza kuwa msimamo wa Moscow juu ya suala hilo haujabadilika.Pamoja na kubainisha tena utayari wa Moscow wa kufanya mazungumzo na Kiev, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amegusia hatua ya Ujerumani ya kuendelea kupeleka silaha Ukraine na akasema: "badala ya Ujerumani kutumia ushawishi wake kwa serikali ya Kiev, inaendelea kuidhaminia Ukraine mifumo mbalimbali ya silaha kinyume na sheria zake yenyewe, ambazo zinakataza kusafirisha silaha nje ya nchi katika maeneo yenye migogoro na mapigano".
Kuhusu kauli za maafisa wa Marekani kwamba Korea Kaskazini imeipelekea silaha Russia kwa ajili ya kuzitumia katika vita vya Ukraine, Zakharova amesema: "haujatolewa na hauwezi kutolewa ushahidi ulio wazi wa kuthibitisha madai haya, kwa sababu maelezo haya ni ya uongo".
Ameyaelezea matamshi hayo ya maafisa wa Washington kuwa ni "kisingizio cha kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini".Vita vya Ukraine pamoja na athari zake mbalimbali za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni, sasa viko katika mwezi wake wa tisa, na nchi za Magharibi bado zinatuma silaha nchini humo.Hatua ya nchi za Ulaya na Magharibi, hasa Marekani ya kuzidisha mashinikizo ya vikwazo dhidi ya Russia na kuipatia Ukraine kila aina ya silaha nyepesi na nzito sio tu haijasaidia kukomesha vita, lakini imezidi kukoleza moto wa mapigano katika nchi hiyo...
342/