Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Novemba 2022

20:37:44
1322188

Faili la pili la sauti ya mwandishi wa BBC: Lengo la ghasia ni kuigawa Iran

Faili la pili la sauti lililovuja la mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limefichua wazi zaidi jinsi televisheni inayofadhiliwa na Saudia inayojiita 'Iran International' inavyoongoza kampeni ya kuigawa Iran vipande vipande.

Ghasia zilizuka Iran wiki za hivi karibuni baada ya Bi. Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22 kuanguka katika kituo cha polisi na kufariki Septemba 16 akiwa anapata matibabu. Ripoti rasmi ya Idara ya Uchunguzi wa Maiti  ilisema kwamba kifo cha Amini kilisababishwa na ugonjwa aliokuwa nao kabla na si kwa kupigwa kichwa au viungo vingine muhimu vya mwili. Ghasia hizo zilikuwa fursa kwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambao wamechochea zaidi ghasia hizo kwa maslahi yao haramu.

Katika ghasia za hivi karibuni, watawala wa Marekani na Ulaya na vyombo vyao vya habari vikiwemo vile vya lugha ya Kifarsi wamechochea ghasia na wale wanaovuruga usalama wa Iran kwa kisingizio cha kuunga mkono haki za binadamu hasa wanawake.

Kuhusiana na njama hizo, Jumapili iliyopita lilivuja faili ya sauti ya Rana Rahimpour  mwandishi wa BBC ya Kifarsi ambapo katika mazungumzo alisikika akisema kubwa lengo la ghasia za Iran si demokrasia bali ni kuwachochea wale wanaotaka kuigawa Iran vipande vipande.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, faili la pili la sauti ya mwandishi huyo limevuja ambapo, mwandishi wa BBC Rana Rahimpour anasikika akifichua zaidi njama hizo kwa kusema: "Nadhani unafahamu nakusudia nini hapa. Nchi za eneo hazitaki kuona Iran ya kidemokrasia." 

Rahimpour anaashiria ghasia mitaani Iran na kusema: "Nilishtuka na kushangaa kutokana na utumiaji mabavu katika ghasia za hivi karibuni. Iwapo hali hii itaendelea, basi nchi itaelekea katika vita vya ndani."

Mwandishi huyo wa BBC amesema televisheni inayofadhiliwa na Saudi Arabia inayojiita 'Iran International' yenye makao yake London, Uingereza imekuwa ikitekeleza njama ya kuchochea maeneo kadhaa yajitenge na Iran. BBC yenyewe haijatafautiana na televisheni ya Iran International katika kuchochea ghasia na kujitenga maeneo ya Iran.

Katika wiki za hivi karibuni, televisheni hiyo ya Kisaudi inayojiita 'Iran International' imekuwa ikisambaza habari za matamshi ya vinara wanaochochea kujitenga baadhi ya maeneo ya Iran yanye kaumu za Wakurdi, Waarabu na Wabaluchi. 

Kwa mfano katika siku 20 za kwanza za ghasia zaidi ya vinara 20 wa makundi yanayotaka kujitenga walihojiwa mara 50 katika televisheni hiyo hasimu. BBC nayo pia haikuachwa nyuma kwani imekuwa ikiwachochea wale wanaotaka kujitenga na Iran na imekuwa ikiunga mkono ghasia na ugaidi nchini Iran.


342/