Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Novemba 2022

20:39:04
1322190

Rais Putin wa Russia kutohudhuria mkutano ujao wa G20

Ikulu ya Rais wa Russia (Kremlin) imesema Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo hatoshiriki mkutano wa kundi la G20 unaotazamiwa kufanyika wiki ijayo mjini Bali nchini Indonesia.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema Rais Putin hatokuwa miongoni mwa viongozi wa mataifa 20 yaliyoendelea kiuchumi duniani watakaohudhuria mkutano huo ujao wa G20, na badala yake atawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov.

Lavrov ataongoza ujumbe wa Russia katika mkutano huo nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani G20, ingawaje baadhi ya duru zinasema yumkini Putin akashiriki mkutano huo kwa njia ya video.

Indonesia imekuwa chini ya mashikizo ya Marekani na waitifaki wake wanaoitaka isimruhusu Rais Putin kushiriki kikao hicho cha siku mbili mjini Bali, wakidai kuwa Russia inapaswa kutengwa kidiplomasia kama adhabu ya kutuma wanajeshi wake Ukraine.

Haya yanajiri wakati huu ambapo Russia na nchi za Magharibi zinaendelea kuvutana na kulumbana juu ya vita vya Ukraine. Februari 24 mwaka huu wa 2022, Russia ilianzisha kampeni maalumu ya kijeshi baada ya kuchochewa na Jeshi la Nchi za Magharibi NATO ambalo liliendelea kurundika wanajeshi wake kwenye mipaka ya Russia na kudharau maonyo yote ya mara kwa mara yaliyotolewa na viongozi wa Moscow.

Hivi karibuni, Waziri Lavrov alisema nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinavuruga usalama wa nchi zote dunia kwa shabaha ya kulinda ubeberu wao.

342/