Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Novemba 2022

20:39:58
1322191

WHO: Vifo vya Corona duniani vimepungua kwa asilimia 90

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametangaza kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Covid-19 ulimwenguni imepungua kwa asilimia 90 katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

  Tedros Adhanom ameeleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kubainisha kuwa mnamo wiki iliyopita, watu 9,400 walifariki kutokana na virusi vya corona duniani kote, kikiwa ni kiwango cha chini mno kulinganisha na idadi ya kila wiki ya vifo katika mwezi Februari, ambayo ilikuwa zaidi ya kesi 75,000.Hata hivyo Adhanom amesema, vifo 10,000 kwa wiki kutokana na ugonjwa unaoweza kuzuilika na unaotibika ni vingi mno na akaongezea kwa kusema: idadi ya vipimo vya corona vilivyofanywa duniani ni ndogo na pengo la chanjo kati ya nchi tajiri na maskini bado ni kubwa.Mkurugenzi Mkuu huyo wa WHO amebainisha pia kwamba, aina mpya za virusi hivyo zingali zinaongezeka na akaongeza kuwa: idadi ya kesi mpya zilizosajiliwa za maambukizi ya Covid-19 ulimwenguni kote imefikia zaidi ya milioni 2.1 wiki hii, ambayo ni pungufu kwa 15% ikilinganishwa na wiki iliyopita.Tedros Adhanom

Idadi kubwa zaidi ya kesi mpya zilizoripotiwa ndani ya wiki hii inahusiana na Japan iliyo na maambukizo zaidi ya laki nne na elfu moja, ambayo inaonyesha ongezeko la 42% ikilinganishwa na wiki iliyopita.Wakati huo huo, China imeshuhudia vifo 539 vilivyosababishwa na Covid-19 katika kipindi cha wiki hii, ambavyo ni ongezeko la 10% kulinganisha na wiki iliyopita.../


342/