Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Novemba 2022

20:40:29
1322192

UNICEF: Mamilioni ya watoto hatarini kuathirika na mafuriko duniani

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa, mamilioni ya watoto katika maeneo mbalimbali ya dunia wanakabiliwa na hatari ya mafuriko.

Taarifa hiyo ya UNICEF imeeleza kuwa, mwaka huu pekee takribani watoto milioni 27.7 duniani kote wameathirika na janga la mafuriko makubwa. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi kubwa ya watoto hao walioathiriwa na mafuriko ni miongoni mwa walio hatarini zaidi na wapo katika hatari kubwa ya vitisho vingi ikiwemo kuzama majini na kufa, kupata magonjwa ya milipuko, kukosa maji safi na salama, utapiamlo, kushindwa kuhudhuria masomo na vurugu.

Kadhalika UNICEF imesema, matokeo ya mafuriko mara nyingi huwa hatari zaidi kwa watoto kuliko hali mbaya ya hali ya hewa iliyosababisha mafuriko hayo.

 

Mwaka huu 2022, mafuriko yamechangia kuongezeka kwa vyanzo vikuu vya vifi vya watoto, kama vile utapiamlo, malaria, kipindupindu na kuhara, imeeleza ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa UNICEF UNICEF nchi zilizoathirika zaidi ni Chad, Gambia, Pakistan, na Kaskazini Mashariki mwa Bangladesh na kiwango wanachikishuhudia cha mafuriko ni cha juu sana kwa zaidi ya miaka 30.

Zaidi ya hayo, Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulionya kwamba baadhi ya jamii zinakabiliwa na uhaba wa chakula na uwezekano wa kukabiliwa na njaa ikiwa msaada wa kibinadamu hautaendelezwa na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hazitaongezwa. 

342/