Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

11 Novemba 2022

20:50:21
1322202

Utawala wa Kizayuni wakataa kukabidhi maiti za Wapalestina 10 waliouawa shahidi

Kamati inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa utawala huo ghasibu unaendelea kuzuia viwiliwili vya Wapalestina kumi waliouawa shahidi.

Kwa mujibu wa chaneli ya habari ya Quds Al-Akhbariya, Kamati ya Wafungwa wa Palestina imetangaza katika taarifa yake siku ya Alkhamisi kwamba Wapalestina hao waliuawa shahidi wakati wa kutiwa nguvuni au walipokuwa vifungoni katika jela za utawala wa Kizayuni na hadi sasa Wazayuni wanakataa kukabidhi miili yao kwa familia zao.Wengi kati ya Wapalestina hao waliuawa shahidi kutokana na sera za utawala wa Kizayuni za kudharau na kupuuza makusudi kuwapatia huduma za matibabu wafungwa hao, suala ambalo limekuwa likiendelezwa kwa uratibu maalumu na utawala wa Kizayuni katika miongo ya hivi karibuni.Baadhi ya wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za israel

Awali Bodi inayoshughulikia Masuala ya Wapalestina waliofungwa na walioachiwa huru ilitangaza kuwa, Wapalestina wapatao 4,700 wakiwemo wanawake 30 hivi sasa wamefungwa katika jela za utawala wa Kizayuni.

Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, maafisa wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamezuia mamia ya maiti za Mashahidi Wapalestina na kukataa kuzikabidhi kwa familia zao, au kuzizika kwenye makaburi ambayo yameandikwa nambari tu juu yake.../ 


342/