Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

12 Novemba 2022

20:21:57
1322533

Wazayuni wakasirishwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa wenye maslahi na Wapalestina

Kamati ya Kupambana na Ukoloni ya Umoja wa Mataifa imepasisha muswada wa Kipalestina ambao ndani yake unataka rai na maoni ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuhusiana na hatua ya utawala wa Kizayuni wa israel ya kuendelea kuikalia kwa mabavu Palestina.

Azimio hilo ambalo limepasishwa katika makao makuuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York ambapo limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake The Hague kueleza haraka rai na mtazamo wake kuhusiana na kukaliwa kwa mabavu kwa muda mrefu ardhi za Palestina, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina ambako kunaelezwa kuwa, ni ukukaji wa haki za Wapalestina pamoja na mustakabali wao.

Riyadh al-Malik, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ametangaza kuwa, nchi 97 wanachama wa Umoja wa mataifa zimeunga mkono muswada huo, mataifa 17 yameuopinga huku nchi nyingine 52 zikijizuia kupiga kura. Utawala haramu wa Israel umechukizwa mno na uamuzi huo wan chi wanachama wa Umoja wa Mataifa wa kuwa pamoja na Palestina. 

Gilad Erdan balozi wa utawala dhalimu wa Israel katika Umoja wa Mataifa sambamba na kutofurahishwa na umauzi huo wa Umoja wa Mataifa amedai kuwa, hatuua ya Wapalestina ya kutaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuingilia kati kadhia hiyo inadhoofidha kila fursa yenye lengo la kuleta maridhiano.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, hadi sasa utawala wa Israel haujachukua hatua yoyote ya kutekeleza azimio nambari 2234 la tarehe 23 Disemba 2016 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. 

342/