Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:50:11
1322826

Trump: Wademokrat wameshinda Seneti kwa kuchakachua

Rais wa zamani wa Marekani ametangaza kuwa chama cha Democratic kimeshinda uchaguzi wa Baraza la Seneti kwa udanganyifu katika uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika hivi majuzi nchini humo.

Baada ya Wademokrat kupata ushindi katika uchaguzi wa Seneti na kupata wingi wa kura katika chombo hicho cha kutunga sheria nchini Marekani, Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani ametangaza kuwa: Kumefanyika udanganyifu katika duru hii ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Congress, na wagombea wa chama cha Republican wameshindwa katika Baraza la Seneti kutokana uchakachuaji wa chama cha Democratic.

Akiashiria kuwa maafisa wa uchaguzi walikuwa wakitaka chama cha Democratic kishinde katika jimbo la Arizona, Trump ameongeza kuwa: "Huu ni ulaghai na udanganyifu katika zoezi la kupiga kura, na hauna tofauti na kujaza masanduku ya kura."

Trump alitoa matamshi hayo saa chache baada ya Seneta wa Kidemokrat, Catherine Marie Cortez Masto, kumpiga mweleka Adam Paul Laxalt wa chama cha Republican huko Nevada. Ushindi wa Catherine Cortez, inakifanya chama cha Democratic kuwa na viti 50 katika Seneti ya Marekani na kudumisha wingi wa maseneta wa chama hicho katika baraza hilo.

342/