Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:52:44
1322829

Vijana wa Ufaransa wapinga marufuku ya hijabu katika maeneo ya umma

Matokeo ya uchunguzi uliofanywa nchini Ufaransa yanaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya vijana wa nchi hiyo wanapinga marufuku vazi la hijabu la Kiislamu katika maeneo ya umma.

Waislamu walio wachache nchini Ufaransa daima wamekuwa wakikabiliana na suala la hijabu na masharti magumu kwa wanawake wenye vazi la hilo la staha kutokana na sheria za kilaiki za Ufaransa.

Siku chache zilizopita, wanawake wawili vijana waliokuwa na vazi la hijabu walipigwa vibaya wakiwa barabarani huku gari la polisi likipita kandokando yao.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa taasisi ya CSA ya Ufaransa, asilimia 56 ya vijana wa nchi hiyo wanapinga marufuku ya vazi la hijabu ya Kiislamu katika maeneo ya umma nchini humo.

Mnamo 2011, Ufaransa ilipiga marufuku vazi la hijabu katika maeneo ya umma, na baada ya hapo nchi zingine za Ulaya kama Denmark, Austria, Uholanzi na Bulgaria pia zilipitisha sheria kama hiyo.

Ufaransa imepiga marufuku vazi la hijabu na kuweka vikwazo vingi dhidi ya Waislamu licha ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya.

Nchi za Ulaya zimezidisha sera za chuki na hujuma dhidi ya Uislamu katika miaka ya hivi karibuni.

342/