Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:53:12
1322830

Jeshi la Ukraine latega pakubwa mabomu katika mpaka wa nchi hiyo na Belarusia

Picha zilizochapishwa zinawaonyesha wanajeshi wa Ukraine wakitega mabomu pakubwa karibu na mipaka ya nchi hiyo na Belarusia.

Kamati ya Masuala ya Mipaka ya Serikali ya Belarusia imetangaza kuwa jeshi la Ukraine linaendelea kutega mabomu katika ardhi inayopakana na mipaka ya Belarusia. Kamati hiyo imechapisha picha ambapo wanajeshi wa Ukraine walionekana Jumatano iliyopita wakitega mabomu karibu na mipaka ya Belarusia. 

Kamati ya Masuala ya Mipaka ya Serikali ya Belarusia iliwahi kutangaza kuwa, wanajeshi wa Ukraine wamelipua karibu madaraja yote katika mipaka ya nchi hiyo na Belarusia huku wakitega mabomu kwenye njia na barabara katika maeneo ya mpakani na Belarusia. 

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Russia imechapisha picha zikiwaonyesha wanajeshi wa nchi hiyo wakipewa mafunzo huko Belarusia na mbinu za kivita na vikosi vilivyoko katika medani za mafunzo nchini humo.  

Rais Alexander Lukashenko wa Belarusia aliwahi kusisitiza kuinga mkono Russia kama muitifaki wa nchi yake.

342/