Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:54:51
1322833

Bidhaa za Iran zinazidi kupata umaarufu barani Afrika

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika amesema: "Inatabiriwa kuwa kwa kasi ya sasa ya ustawi wa biashara ya Iran na Afrika katika mwaka huu (1401 Hijria Shamsia) kiwango cha mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika kitafika dola bilioni 1.8.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRNA, Sayyid Ruhullah Latifi, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika, katika kipindi cha miezi saba iliyopita, mauzo ya Iran barani Afrika yamefika dola milioni 912 katika nchi 37.Ameongeza kuwa: "Katika miezi saba iliyopita, mabadilishano ya kibiashara ya tani milioni 1 laki 851 na elfu 911 zenye thamani ya dola milioni 972.9 yalifanyika kati ya Iran na nchi za Afrika, ambapo tani milioni 1. 787 zenye thamani ya dola milioni 912. 1 zilikuwa sehemu ya mauzo ya Iran kwa nchi 37 za Afrika na takribani tani elfu 65.1 za bidhaa zenye thamani ya dola milioni 60.8 zimeingizwa nchini kutoka nchi 20 za Afrika."

Kuhusu maeneo matano ya juu zaidi ya mauzo ya bidhaa za Iran katika bara la Afrika, Latifi alisema: Afrika Kusini, Msumbiji, Sudan, Nigeria na Ghana zilikuwa nchi tano bora za mauzo ya bidhaa za Iran katika bara la Afrika katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika ameongeza kuwa, Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Ghana na Kongo ndizo nchi tano za Kiafrika zinazoongoza katika kuiuzia Iran bidhaa.

342/