Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:58:14
1322836

Wanamfalme wa Saudia na biashara ya madawa ya kulevya Mashariki ya Kati

Duru moja nchini Saudi Arabia imeripoti kuhusu kuongezeka matumizi ya madawa ya kulevya na kuhusika wanamfalme wa nchi hiyo katika kuingiza nchini mihadarati.

Takriban hakuna nchi iliyosalimika na janga la madawa ya kulevya hata hivyo kile ambacho kinaitofautisha Saudi Arabia katika eneo la Mashariki ya Kati ni kuhusika rasmi makademu,  wanamfalme na maafisa wa nchi hiyo katika kusafirisha na kuingiza nchini kiasi kikubwa cha mihadarati.  

Tovuti ya habari ya al Khalij al Jadid imeripoti kuwa, Saudi Arabia kati ya mwaka 2015 hadi 2019 ilichangia upatikanaji wa zaidi ya asilimia 45 ya  dawa aina ya Amphetamine kwa jina jingine Captagon huku watu wa familia ya ukoo huo wa kifalme na askari usalama wakihusika katika kusambaza dawa hizo.  

Makadirio rasmi yaliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia yanaonyesha kuwa jumla ya watu laki mbili wameathiriwa na  madawa ya kulevya nchini humo. 

Wakati huo huo Saudi Arabia ni nchi ya tatu kwa matumizi ya mihadarati duniani na nchi inayotumia pakubwa dawa za kulevya katika eneo la Asia Magharibi.

Aidha kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo, mtu anayetumia na kuuza madawa ya kulevya huhukumiwa kunyongwa hata hivyo sheria hiyo hutekelezwa kwa raia wa kawaida na wahamiaji na si kwa watu wa familia ya kifalme ambao hawaguswi na mkono wa sheria. 

342/