Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:58:40
1322837

Hamas yasisitiza kutekeleza Tangazo la Algeria na kuhitimisha hitilafu za ndani

Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa harakati hiyo ipo tayari kutekeleza Tangazo la Algeria kuhusu mapatano ya kitaifa na kuhitimisha hitilafu za ndani.

Abu Marzouq amesisitiza kuwa, Hamas ina hamu na iko tayari ili kuhakikisha kuwa umoja wa kitaifa unapatikana na Tangazo la Algeria linatekelezwa. Amesema, marhala ya sasa inahitaji kumaliza hitilafu zote zilizopo na kujikita na mapambano dhidi ya utawala ghasibu. 

Ujumbe wa Hamas umeashiria mashambulizi ya kila uchao ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mauaji ya Wapalestina yanayofanywa na wanajeshi ghasibu wa Israel na kusema: chaguo la mapambano ni chaguo bora zaidi la kukabiliana na utawala haramu wa Israel na kushinda njama zake. 

Makundi ya Palestina Alhamisi iliyopita usiku yalifanya kikao huko Algeria cha kufunga "Mkutano wa Maridhiano ya Kitaifa ya Palestina. Makundi hayo ya Kipalestina yalipongeza mchango na msimamo wa Algeria na rais wa nchi hiyo katika kuyaunganisha pamoja makundi na msimamo wa nchi hiyo wa kuunga mkono kadhia ya Palestina.  

Makundi ya Palestina yamesaini Tangazo hilo la Algeria na yametilia mkazo umuhimu wa umoja wa kitaifa kama msingi mkuu katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni. Yamesisitiza pia umuhimu wa kushiriki kisiasa makundi ya Palestina kupitia uchaguzi.

342/