Waziri wa Vikosi vya Majeshi ya Uingereza, James Heappey ameliambia Bunge la nchi hiyo kuwa, serikali ya London haiwezi kuvumilia udhalilishaji wa nchi mwenyeji, ambayo eti haina azma ya kushirikiana na nchi hiyo ya Ulaya kurejesha uthabiti na usalama wa kudumu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Amesema wimbi la mapinduzi yaliyoshuhudiwa hivi karibuni nchini Mali linakwamisha jitihada za kimataifa za eti kupambana na ugaidi nchini humo, na kwa msingi huo Uingereza itawaondoa wanajeshi wake 300 katika nchi hiyo ya eneo la Sahel barani Afrika.
Hii ni katika hali ambayo, mabaki ya wanajeshi wa Ufaransa waliondoka nchini Mali Agosti mwaka huu, kuashiria mwisho wa Operesheni ya Barkhane katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Vikosi vya wanajeshi 2,400 wa Ufaransa vimekuwepo nchini Mali kwa takriban miaka 10 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Kikosi cha MINUSMA kina askari wapatao 14,000.
Viongozi wa kijeshi walioko madarakani nchini Mali tangu mwezi Agosti mwaka 2020 waliamua kusitisha ushirikiano na Ufaransa na nchi nyingine za Magharibi, na sasa wanashirikiana na Russia katika vita dhidi ya magaidi.
342/