Main Title

source : Parstoday
Jumanne

15 Novemba 2022

16:46:26
1323366

Hizbullah: Marekani imekusudia kuingamiza kabisa Lebanon

Naibu wa Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inapanga njama za kuiangamiza kabisa kabisa Lebanon.

Tovuti ya al Nashra imeripoti habari hiyo na kumnukuu Sheikh Ali Da'mush akisema hayo jana Jumapili na kusisitiza kuwa, muqawama hivi sasa ni imara na una nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote na kwa taufiki ya Allah na jitihada kubwa na baraka za damu za mashahidi, leo hii tunaiona Lebannon ikiwa nchi yenye nguvu na inayoamua mambo yake na kuyatekeleza bila ya woga.

Ameongeza kuwa, mafanikio iliyopata hivi karibuni Lebanon ya kuulazimisha utawala wa Kizayuni ufanye haraka kushiriki katika uchoraji wa mipaka ya baharini na kukubali masharti ya Beirut, kwa hakika ni ushindi mkubwa kwa taifa la Lebanon. Amesema, mafanikio hayo makubwa yasingeliweza kupatikana kama si kwa taufiki ya Allah na mshikamano baina ya Serikali, Muqawama na wananchi wa Lebanon. 

Amma kuhusu wasiwasi wa kutoheshimu Wazayuni makubaliano hayo ya kuchorwa mipaka ya baharini kwa kuingia madarakani serikali ya kifashistri huko Tel Aviv, kiongozi huyo mwandamizi wa harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema, Benjamin Netanyahu hana uthubutu wa kuvunja makubaliano hayo. Ametoa sababu ya jambo hilo kwa kusema: Moja ya sababu hizo na ambayo ni muhimu zaidi ni kwamba taasisi mbili za kijeshi na kiusalama za Israel zote zinakubaliana kuhusu umuhimu wa makubaliano hayo kwa usalama wa utawala wa Kizayuni na kuepusha kutokea vita baina ya Lebanon na Israel.

Amesema, madhali muqawama una nguvu huko Lebanon, utawala wa Kizayuni hauthubutu kuifanya lolote nchi hiyo ya Kiarabu.

342/