Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:17:13
1323735

Russia: Kilichotokea Poland ni ithibati kuwa Magharibi inakaribia zaidi kuanzisha Vita vya Dunia

Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia ametahadharisha juu ya kuzuka vita vya dunia kufuatia tuhuma zilizotolewa na Magharibi dhidi ya Moscow katika tukio la kombora lililoangukia ndani ya ardhi ya Poland.

Radio Zeit ya Poland ilitangaza jana usiku kuwa makombora mawili yamepiga kijiji cha Przewodów katika eneo la Lobelski Voivodeship mashariki mwa nchi hiyo kwenye mpaka wa pamoja na Ukraine na kwamba watu wawili wameuawa katika tukio hilo.Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Taifa la Russia, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: "tukio la 'shambulio la kombora' kwenye shamba moja huko Poland linathibitisha jambo moja tu: kwa kuendesha vitamseto dhidi ya Russia, Magharibi inakaribia zaidi kuanzisha Vita vya Dunia".Rais Andrzej Duda wa Jamhuri ya Poland, ametangaza leo katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, maafisa wa serikali hawana taarifa za uhakika kwamba ni nchi gani imerusha kombora lililoangukia mashariki mwa nchi hiyo, lakini kuna uwezekano kuwa kombora hilo limetengenezwa Russia.

Hii ni katika hali ambayo katika ripoti za awali, afisa mmoja wa intelijensia wa Marekani amedai katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press kuwa, makombora ya Russia yamedondokea nchini Poland.

Saa chache baadaye, Associated Press iliwanukuu maafisa watatu wa Marekani na kuripoti kuwa: tathmini ya awali inaonyesha kwamba kombora la ulinzi wa anga la Ukraine ndilo lililoangukie kwenye ardhi ya Poland.Baada ya kutokea ajali hiyo, Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza kuwa kuzungumza kwamba ardhi ya Poland imelengwa na kombora ni hatua ya makusudi ya kuanzisha chokochoko.../


342/