Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:21:55
1323743

Mkuu wa IRIB: Licha ya kuwekewa vikwazo, sauti ya Jamhuri ya Kiislamu itawafikia walimwengu

Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) amesema: Kanali ya Press TV inaendesha shughuli zake katika uga wa kimataifa licha ya kukabiliana na washindani wenye nguvu; na licha ya kuwekewa vikwazo, sauti ya Jamhuri ya Kiislamu itawafikia walimwengu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, Peyman Jebeli, Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo pembeni ya kikao cha Baraza la Mawaziri na kuongeza kuwa: Kanali ya Press TV inafanya kazi katika uga wa kimataifa licha ya kuwepo washindani wenye nguvu, lakini Wamagharibi hawawezi kuvumilia hata uwepo wa kiwango cha chini wa nyenzo na suhula wa televisheni hiyo.

Jebeli ameeleza kuwa inachofanya Magharibi ni kinyume na madai yake ya kuheshimu uhuru wa kutoa maoni na kujieleza, na akasisitiza kuwa: kwa upande wa programu na matangazo, Press TV inatoa ushindani mkali kwa kanali za kimataifa za habari; na licha ya kuwekewa vikwazo, sauti ya Jamhuri ya Kiislamu itawafikia walimwengu.

Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa: kwa vile redio na televisheni za matangazo ya ng'ambo ya Iran zina tajiriba, uzoefu na utayarifu unaohitajika, hapana shaka zitaivuka hali ya sasa iliyopo.Siku ya Jumatatu, Umoja wa Ulaya na Uingereza zilitangaza kuiwekea vikwazo vipya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hatua iliyopangwa na kuratibiwa baina ya pande mbili hizo.Vikwazo hivyo vilivyohusisha shakhsia zaidi ya 20 na asasi kadhaa za Iran vimejumuisha pia kanali ya televisheni ya Press TV.../


342/