Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:22:30
1323744

Abdollahian: Iran katu haitawaruhusu magaidi kuchezea shere usalama wake

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi wa Iran katu hatawaruhusu usalama na maslahi ya nchi yao kuchezewa shere na madola ya Magharibi na magaidi wanaopatiwa misaada na madola hayo.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo katika barua yake kwa Ivica Dacic, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Serbia ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na kueleza kwamba, inasikitisha kuona kuwa, kuna baadhi ya madola yanadai kupambana na ugaidi lakini siasa zao zinashajiisha na kuchochea vitendo vya fujo, vurugu na utumiaji mabavu.

Aidha katika barua yake hiyo kwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Serbia, Hussein Amir-Abdollah ameashiria mafanikio ya ushirikiano wa Iran na madola huru ikiwemo Jamhuri ya Serbia katika kuchukua hatua za kupambana na ugaidi. 

Kadhalika Abdollahian ameeleza katika barua hiyo kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mmoja wa wahanga wa vitendo vya ugaidi na misimamo ya kufurutu ada na kwamba, daima imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na matukio haya mabaya na kulieleza bayana hilo katika majukwaa ya kieneo na kimataifa.

Amesema pia kuwa, madola ya Magharibi yanayodai kupambana na ugaidi na ambayo yamekata tamaa ya kufikia malengo yao baada ya kufelii na kugonga mwamba siasa zao za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa, sasa yanafanya njama za kutumia siasa za majitaka na hadaa kama vile kushajiisha na kuchochea vurugu na machafuko sambamba na mauaji ili kutia dosari na kuikwamisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika njia yake ya kupiga hatua kuelekea katikak ustawi, maendeleo na kujiimarisha zaidi.

342/